Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)(Picha na Maktaba)
Baraza
la Sanaa la Taifa, BASATA limeitaka kamati ya Miss Tanzania
iliyojiuzulu mapema mwaka huu kukaa chini na waandaji wa shindano hilo,
Lino Agency kumaliza tofauti zao.
Kupitia Twitter BASATA limeandika:
BASATA
imeitaka kampuni ya LINO waandaaji wa Miss Tanzania kurudi mezani na
kamati ya shindano kujadiliana namna bora ya kusonga mbele. Imeiagiza
LINO kuandaa MoU na kamati ya shindano la Miss Tanzania ili kuchora
mipaka ya kiutendaji baina yao.
Kama
ya shindano la Miss Tanzania, ilitangaza kujiuzulu kwa kile mwenyekiti
wa kamati ya maandilizi ya shindano hilo Juma Pinto, kudai ni kutokana
na kushindwa kujua nini majukumu yao na yale ya kampuni inayoyaanda,
Lino.
Alidai kuwa awali iliwekwa wazi kuwa ni kamati hiyo ndiyo itakayoratibu mashindano hayo huku Lino Agency ikibaki kuwa washauri.
Pinto
alisema Lino imeendelea kufanya kazi yake lakini wao wakibaki bila
kujua kinachoendelea. “Sisi tumeona tuje tuzungumze tu kwamba sisi
hatupo huko,” amesema Pinto.
Naye
msemaji wa kamati hiyo, Jokate Mwegelo alisema kutokana na ukubwa wa
kile Miss Tanzania imefanya kwa wasichana, wasilichukulie kwa wepesi na
kiubinafsi.
“Waangalie
wasichana wa Tanzania wanawatoaje? Na kuwatoa ni kuhakikisha kwanza
misingi ya shindano lenyewe iwe ya kueleweka. Kama misingi haieleweki
ndio tunarudi kule kule,” amesema Jokate.
Aliongeza kuwa makosa yaliyojitokeza miaka iliyopita pamoja na malalamiko mengi dhidi ya shindano hilo yanapaswa kufanyiwa kazi.
0 comments:
Post a Comment