Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WASANII KUNUFAIKA NA MFUMO MPYA WA UONYESHWAJI FILAMU

WASANII KUNUFAIKA NA MFUMO MPYA WA UONYESHWAJI FILAMU

s1 
Msemaji kutoka kituo cha Sibuka Televisheni wa kwanza kulia   Bw. George Nangale  akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo hiko cha matangazo uliofanyika leo jijini Dar es salaam, kushoto ni Afisa habari wa kampuni ya Step Entertainment  Bw. Moses Mwanyilu.
s2Mkurugenzi wa matamasha  kutoka kampuni ya usambazaji filamu nchini Steps Entertainment katikati Bw. Jonas Sabuni akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” ambao uliofanyika leo jijini Dar es salaam,  kushoto ni Afisa habari wa kampuni hiyo Bw. Moses Mwanyilu na kulia ni mwigizaji wa bongo movie Jimmy Mafufu.
s3 
Afisa habari wa kampuni ya Step Entertainment  Bw. Moses Mwanyilu wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo cha matangazo Sibuka Televisheni uliofanyika leo jijini Dar es salaam,katikati ni , Msemaji kutoka kituo cha Sibuka Televisheni  Bw. George Nangale na wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Masoko kutoka Startimes Bw. Awino Felia.
s4 
Meneja Masoko kutoka Startimes Bw. Awino Felia  wa kwanza kushoto akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kipindi cha INABAMBA “Ni bongo movie bandika bandua” kitachokuwa kinaonyeshwa katika kituo cha matangazo Sibuka Televisheni kupitia king’amuzi cha Startimes  uliofanyika leo jijini Dar es salaam
PICHA ZOTE NA ALLY DAUD-MAELEZO.

Na Beatrice Lyimo MAELEZO Dar es Salaam
WASANII wa Filamu nchini wanatarajia kunufaika na kazi zao kufutia makubiliano ya Kampuni ya Star Media Tanzania Ltd (Startimes), pamoja na Steps Entertainment za kutumia kazi zao kwenye vituo vya televisheni nchini.
Akizungumza waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa  Sibuka Media, Dkt. George Nangale  alisema kazi hiyo itafanywa kwa ushirikiano na taasisi hizo ili kuweza kuwasaidia wasanii kunufaika na kazi zao kupitia luninga badala ya kuwasubiri  wateja wao kuzinunua katika santuri (DvD).
“Tumefikia uamuzi huu baada ya kuona ombwe lililopo sasa katika kuzifikisha filamu zetu kwa walio wengi pamoja na kwamba Watanzania wana mwamko mkubwa wa kuzitazama filamu hizi zenye mafunzo ya maisha na burudani” alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Kwa upande wake Msanii wa Bongo Movie, Mwanaheri Hamad alisema uonyeshaji wa kazi zao katika vituo vya televisheni utawanufaisha wasanii chipukizi ambao kazi zao bado hazijaonekana.
Amesema kuwa kutokana na mkataba huo wa kurusha filamu hzo umerahisisha soko za kazi hizo katika mfumo DvD ambapo ulikuwa unatumiwa hapo awali.
Filamu hizo zitaonyeshwa kupitia king’amuzi cha StarTimes chaneli 111 ikijulikana kama Sibuka Maisha Steps chaneli kila siku na itaanza kuonyeshwa Ijumaa hii tarehe 29 Julai, 2016.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa