Diwani
wa Kata ya Ilala, Saady Khimji ametoa wito kwa Serikali na Mashirika
binafsi kuisaidia Kampuni ya Dar Festival ili Iweze kufanya tamasha la
kutangaza utamaduni wa nchi ya Tanzania.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Diwani huyo ambaye pia ni Mlezi
wa Kampuni hiyo alipokuwa akilitangaza rasmi tamasha hilo mbele ya
waandishi wa habari.
Khimji
amesema kuwa ni jambo jema kuona vijana wanazungumzia suala la
utamaduni kwani hali hii inaonyesha dhahiri kuwa wameamua kuirudisha
nchi kwenye mstari wa kujali utamaduni wetu.
“Mataifa
yote makubwa yanajali tamaduni zao hivyo ni vema na sisi kama
watanzania kuamua kwa dhati kuhakikisha tunarudisha utamaduni wetu,
jambo hili sio dogo linahitaji fedha nyingi kwahiyo, tunaomba msaada
kutoka kwa Serikali na Mashirika binafsi ili kufanikisha tamasha hili”,
alisema Khimji.
Diwani
huyo ameongeza kuwa vijana hao wamejitahidi hadi hapo walipofika lakini
kama wakikosa misaada kutoka kwa wadhamini mbalimbali basi tamasha hilo
halitoweza kufanikiwa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Faridi Faradji amesema kuwa
wameamua kuisaidia Serikali kwa kuangalia njia mbadala ya kukusanya
mapato kwa kutangaza utamaduni wa Tanzania kupitia tamasha hilo.
“Kwa
namna moja au nyingine,tuna kila sababu ya kuisaidia nchi yetu
kukusanya mapato ili iweze kuendelea kwasababu baadhi ya nchi zingine
zimeweza kuendelea kupitia matamasha kama haya”, alisema Faradji.
Naye
Katibu wa Kampuni hiyo, Amini Kingazi amesema kuwa tamasha hilo ni la
asili kwahiyo wameamua kulifanyia katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa
kwa sababu ni eneo lenye vitu vingi vinavyoonyesha utamaduni wa
kitanzania.
Tamasha
hilo linatarajiwa kufanyika kila mwaka, Kwa mara ya kwanza litafanyika
mwezi Septemba mwaka huu likijumuisha vitu vyenye asili ya kitanzania
kama vyakula vya kitanzania, mashindano ya michezo ya kiasili pamoja na
wanamuziki wa kitanzania.
0 comments:
Post a Comment