Profesa Mbarawa:
Serikali haijakurupuka kununua ndege za Bombadier Q400
Na
Abushehe Nondo na Sheila Simba.
MAELEZO
Dar
es Salaam
Serikali imesema
kuwa iliamua kununua ndege mbili za abiria aina ya Bombadier Q400 kutoka nchini
Canada kutokana na uhitaji wa huduma ya usafiri wa anga kwa safari za ndani ya
nchi na mazingira halisi ya viwanja vya ndege vilivyopo nchini.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Profesa Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wakufunzi wa marubani
katika chuo cha Taifa cha usafirishaji(NIT)
Mbarawa
alisema kuwa Serikali haikukurupuka katika kufanya maamuzi ya aina ya ndege za
kununua badala yake imezingatia vigezo na malengo mahsusi ya kuhudumia usafiri
wa ndani na kuboresha usafiri wa anga kupitia Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).
“Serikali
imeamua kununua aina hii ya ndege za Bombadier Q400 kutokana na hali halisi ya
Viwanja vya ndege nchini kuwa vya Changarawe na lami kwa baadhi, huku lengo ni
kutoa huduma za usafiri wa ndani” Alisema Profesa Mbarawa.
Mbarawa
aliwataka Watanzania kuelewa nia ya Serikali yao ni kuhudumia wananchi hivyo
watu wasipotoshe ukweli kuhusu ndege hizo kwani zimezingatia mambo mbalimbali
ikiwemo suala la usalama na ufanisi katika uendeshaji wake.
Aliongeza
kuwa ndege hizo zina uwezo wa kutua katika viwanja vingi hapa nchini kwani zinaweza
kutua katika viwanja vyenye urefu wa kilomita 1.5 ambavyo ndio vingi nchini tofauti
na aina nyingine ambazo hutua kwenye viwanja vyenye urefu zaidi ya kilomita
mbili.
Prof.
Mbarawa alibainisha sababu nyingine kuwa ni aliongeza uwezo mdogo wa ndege hizo
katika kutumia mafuta ukilinganisha na aina zingine ambapo kwa safari ya kutoka
Dar es Salaam hadi Mwanza zitakuwa zikitumia Tani 1.7 za mafuta tofauti na aina
nyingine zinazotumia hadi Tani 2.8 kwa safari moja.
Waziri
Mbarawa pia alitumia fursa hiyo kukanusha uvumi ulionezwa kuwa ndege hizo
zimenunuliwa katika kampuni ndogo isiyokuwa na sifa na kubainisha kuwa suala
hilo siyo la kweli kwani kampuni hiyo imefanya biashara na nchini nyingi
ikiwemo Ethiopia yenye ndege t19 aina ya Bombadier Q400 zilizotengezwa na Kampuni hiyo.
Mpaka
sasa tayari Serikali imeshafanya malipo ya ununuzi wa ndege hizo kwa asilimia
40 ambapo ndege hizo zinatarajiwa kuwasili nchi tarehe 19 septemba mwaka huu ambapo
zitaanza safari ya kutoka nchini Canada tarehe 15 septemba mwaka huu kupitia nchini
Uingereza.
Akizindua
mafunzo hayo ya wakufunzi wa marubani,
Waziri Mbarawa aliwaasa Marubani ambao watahitimu mafunzo hayo kuhakikisha wanazingatia suala na nidhamu na
uadilifu katika sekta hiyo ya usafiri wa anga.
“Hatutaki
kuwa na marubani ambao wana uwezo wa kazi lakini sio waadilifu,hakikisheni
mnawafundisha marubani wanafunzi kuzingatia nidhamu na uadilifu katika sekta
hiyo ya anga ambapo wakati mwingine Rubani anajijua anakasoro lakini bado
anang’ang’ania kurusha ndege” alisema Prof.Mbarawa.
Aidha
amesema kuwa Serikali itashirikiana na chuo hicho katika kutoa kozi za urubani
ili kuakabiliana na changamoto ya ukosefu wa marubani nchini.
MWISHO
1 comments:
Asante kwa ufafanuzi tulikuwa tunapotoshwa na wasio na taarifa Halisi . Tuishukuru serikali kwa kujibu na kuutolea ufafanuzi uvumi
Post a Comment