Serikali,kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali leo imefanya kikao
maalumu cha wadau kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na asasi za
kiraia kwa lengo la kuwafahamisha kuhusu kujadiliwa kwa Taarifa ya pili
ya nchi ya utekelezaji wa masuala ya Haki za Binadamu chini ya mfumo wa
mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Period Review).
Vilevile
kikao hicho kitatoa fursa ya kujadili kwa kina na kuyapatia misismamo
ya awali kama wadau, mapendekezo yaliyotolewa na Baraza la Haki za
Binadamu la Umoja wa Mataifa kwa Serikali mnamo mwezi Mei 2016 , na
kuainisha sababu ambazo zinafaa kwa mapendekezo yaliyoahirishwa kwa
maslahi mapana ya nchi yetu kabla ya kupitishwa rasmi kuwa taarifa ya nchi itakayowasilishwa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kabla ya terehe 9 Septemba 2016.
Akifungua
kikao hicho Mkurugenzi wa masuala ya Katiba na Haki za Binadamu kutoka
Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali, Bi Sarah Mwaipopo ameeleza kuwa
kikao hicho ni hatua muhimu kkatika mfumo wa maandalizi ya taarifa za
usimamizi na utekelezaji wa haki za binadamu nchini ambao umekua
ukishirikisha wadau wote kutoka Wizara,Idara na Taasisi za Serikali
pamoja na Taasisi zisizo za kiserikali ambapo amesisitiza wadau wote
kuendelea kutoa ushirikiano na kutimiza wajibu wao ipasavyo.
“Sote
tutambue na kuzingatia kwamba masuala ya haki za biandamu ni mtambuka
na kila mtu ana wajibu wa kutekeleza na kuyasemea katika eneo lake”alisema Bi Sarah
Halikadhalika,kwa niaba ya Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekua ikiratibu kikamilifu maandalizi na uwasilishwaji wa Taarifa zote za masuala yote ya haki
za binadamu kwa kuzingatia mikataba ya Haki za Binadamu ambayo Tanzania
imeridhia na utekelezaji wa jukumu hili umeanishwa katika Ibara ya
59(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 na Sheria ya
Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Sura ya
268, kifungu cha 14(f) ambayo ni;
kuratibu
masuala ya uaandaaji na utoaji wa taarifa za nchi za utekelezaji wa
Mikataba ya Kikanda na Kimataifa ya haki za binadamu amabyo nchi
imeridhia ikiwemo masuala yote ambayo yanahitaji utolewaji wa taarifa za
aina hiyo na kuziwasilisha kwenye vyombo husika vya Kikanda na
Kimataifa kwa ajili ya majadiliano.
Kikao
hicho ambacho kitafanyika kuanzia tarehe 30 -31 Septemba 2016 jijini
Dar es Salaam kimehudhuriwa na wadau kutoka Tanzania Bara na Zanzibar
ambao ni Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jukwaa la
Katiba Tanzania,Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania,MISA-TAN,PINGOS’
FORUM,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Wizara ya Katiba na Sheria,
Mahakama ya Tanzania,Uhamiaji,Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora,
Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA), Shrikisho la Watu wenye ulemavu
Tanzania( SHIVYAWATA) na Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali. Kwa
upande wa Zanzibar ni Wizara ya Kilmo na Mifugo, Wizara za Afya,Mifugo,
Kazi,Vijana Wazee,Ofisi ya Mwansheria Mkuu, Jumuia ya Wanawake
Wanasheria,Tume ya Uchaguzi
Utaratibu
wa Mapitio kwa kipindi maalum (The Universal Periodic Review) wa
masuala ya haki za binadamu ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka
2006 kwa lengo la kuzifanyia mapitio nchi 192 ambazo ni wanachama wa
Umoja wa Mataifa, Tanzania ikiwa miongoni, kwa lengo la kuangalia
utekelezaji wa masuala ya kulinda na kukuza haki za binadamu nchini
mwao.
0 comments:
Post a Comment