Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » RAIS MAGUFULI AMEFANANA NA YOHANA MBATIZAJI: MAKAMBA

RAIS MAGUFULI AMEFANANA NA YOHANA MBATIZAJI: MAKAMBA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 



Na  Immaculate Makilika –MAELEZO

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Yusuph Makamba alisema kuwa  Rais Magufuli anafanana na Yohana Mbatizaji kwa vile ni kiongozi  anayefanyakazi bila kuogopa.

Makamba ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu katika mahojiano maalum na  Mwandishi  wa habari hizi.

Makamba alisema kuwa  Rais ni kiongozi mchapakazi ambaye hayumbushwi na maneno wala vitisho  kwa vile anasema ukweli katika kutekeleza majukumu yake.

“Yohana Mbatizaji alisema ukweli na hakutikiswa na upepo, hakuogopa macho ya watu wala hakuwa mtu wa majigambo, kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu Marko 6:12, na hivyo ndiyo navyomfananisha Rais wetu Magufuli na viongozi wote tumuunge mkono” alisema Makamba.

Aidha, kuhusu maika 55 ya Uhuru , alisema kuwa ni vyema Watanzania  wakazingatia wito wa uhuru ni kazi, na kwa kuwa Serikali hii imeweka mkazo katika ufanyaji kazi.

Makamba  alisema kuwa katika Awamu hii ya HAPAKAZI TU, inaakisi wito wa Uhuru katika vipindi mbalimbali kuanzia kipindi cha Uhuru ni kazi na Uhuru na kazi mara baada ya kupatikana kwa Uhuru  na kuwakumbusha  watanzania kuulinda Uhuru.

“Ni lazima kuulinda Uhuru kwa gharama yeyote ili amani na mshikamano uendelee kuwepo basi hatuna budii kuepuka lugha zenye  maneno ya uchochezi, ukabila na udini” alisema Makamba

mwisho

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa