Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Fili Karashani, mwandishi mkongwe aliyeshinda tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Tasnia ya Habari mwaka 2011, katika tuzo za (EJAT) zilizoandaliwa na Baraza la Habari Nchini Tanzania (MCT) na washirika wake, hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jana usiku, Kushoto ni Mwandishi wa siku nyingi Khamis Ben Kiko.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi mwandishi, Nevil Meena, cheti cha ushindi wa jumla katika tuzo hizo baada ya kutangazwa rasmi.
Kikundi cha Ngoma za asili cha Simba Thietre kikitumbuiza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Teddy Mapunda akikabidhi tuzo kwa mwandhishi wa habari wa Mlimani Radio Tuma Dandi aliyeibuka mshindi wa habari za watu wenye ulemavu- kwa upande wa Redio.
Mhariri wa gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda(kulia) akikabidhi tuzo kwa Abdallah Majura Mkurugenzi wa Radio Sports FM ya Dodoma..
Mkurugenzi wa kampuni ya Executive Solution, Agrey Maleale, akimkabidhi zawadi Khamis Hamad kutoka magazeti ya Uhuru na Mzalendo, kwa kuibuka mshindi wa Tuzo ya mpiga picha Bora wa mwaka 2011-2012.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi walipokutana katika hafla hiyo.
0 comments:
Post a Comment