Home » » CHAMA CHA MAPINDUZI CHAMPONGEZA JOSHUA NASARI MBUNGE MTEULE WA ARUMERU MASHARIKI

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAMPONGEZA JOSHUA NASARI MBUNGE MTEULE WA ARUMERU MASHARIKI


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye akiongea na
waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama hicho zilizopo mtaa
wa lumumba jijini Dar es salaam,  juu ya uchaguzi mdogo wa ubunge
ulifanyika jana katika jimbo la Arumeru mashariki, ambapo mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari ameibuka mshindi kwa kura 32.972, chama cha mapinduzi kimekubali
 matokeo hayo yaliotangawa na Tume ya uchaguzi leo asubuhi 


Nape kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza kijana Nasari na kusema "Tunampongeza Joshua Nasari na hakuna hujuma yoyote uchaguzi ulikuwa huru na haki", lakini pia akawapongeza wananchi wa jimbo la Arumeru kwani hiyo ndiyo Demokrasia yao.

Baandhi ya wandishi wa habari walioudhuria katika mkutano huo leo wakimsikiliza Nape Nnauye alipokuwa akiongea nao juu ya uchaguzi huo..
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Habari na Full Shangwe Blog



0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa