Home » » Kiwanda cha Magunia Chawaka Moto jana

Kiwanda cha Magunia Chawaka Moto jana


MOTO mkubwa umezuka jana katika Kiwanda cha kutengenezea magunia cha Tasipa kilichopo 
Urafiki Ubungo, Dar es Salaam na kuteketeza asilimia kubwa ya magunia yaliyokuwamo katika ghala la kutunzia bidhaa. 

Moto huo ambao chanzo chake hakikujulikana, ulianza saa nne asubuhi na pia uliziathiri familia kadhaa zinazoishi jirani na kiwanda hicho kilichopo katika makazi ya watu. 

Akizungumza na gazeti hili katika eneo la tukio, Mkurugenzi Msaidizi wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China, Ray Rong alisema moto ulianzia katika sehemu ya ghala hilo na ulikuwa kidogo hivyo alishirikiana na wafanyakazi wa kiwanda hicho kuuzima bila ya mafanikio. 

Naye Ofisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji cha Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kiwanda hicho hakina vifaa vyovyote vya kuzimia 
moto, lakini pia hakina cheti kinachothibitisha kuwa kimekaguliwa na Idara ya Zimamoto. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela hakupatikana kuzungumzia ajali hiyo, na 
gazeti hili lilibaini hakuna madhara kwa binadamu.
Chanzo Habari Leo

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa