Home » » NMB FINANCIAL FITNESS MASHULENI

NMB FINANCIAL FITNESS MASHULENI

Benki ya NMB hivi karibuni Ilizindua
mpango wa kukuza uelewa wa maswala ya kifedha kwa wanafunzi mashuleni
unaoitwa NMB Financial Fitness, uzinduzi wa awali ulifanyika katika shule
ya sekondari Pugu tarehe 17 Mei 2012 na baadae kuingia katika shule za msingi mbalimbali jijini Dar es salaam.

Mpango wa NMB Financial
Fitness unalengo la kuongeza uelewa wa matumizi mazuri ya kifedha, uwekaji
akiba, kujenga uwezo wa kupanga matumizi na mengine mengi.

Baada ya uzinduzi ,
Benki ya NMB imeendelea kutambulisha mpango huu kwenye Kanda ya Dar
es Salaam katika shule mbalimbali kama utakavyoona picha mbalimbali zilizopigwa katika shule za jiji la Dar es salaam.

Wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge wakijisomea jarida
ya NMB Financial Fitness.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Hananasifu wakijisomea jarida la NMB
Wanafunzi wa shule ya msingi Tandika wakiwa wameinua
jarida lao ya NMB Financial Fitness
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya Ilala Boma
wakiwa makini kusoma jarida la NMB Financial Fitness.
Afisa Benki ya NMB akiwaelekeza jambo wanafunzi wa
shule ya msingi ya Mapambano
Wanafunzi wa Turiani wakiwa katika picha ya pamoja
na Maafisa wa Benki ya NMB pamoja na mwalimu wao.
Wanafunzi wa shule ya msingi Hananasifu wakisoma jarida la NMB Financial
Fitness.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa