Home » » Phares Magesa:Pongezi Kwa Wanataaluma Walioteuliwa kuwa Wabunge

Phares Magesa:Pongezi Kwa Wanataaluma Walioteuliwa kuwa Wabunge

 Phares Magesa,Rais- Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN)
--
Wazalendo wanzangu,

Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Rais wa Jamhuru ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk. Jakaya M. Kikwete kwa kuwateua wanataaluma  Mhe. Janet Mbene (M.Sc - Economics)  na Mhe. Prof. Sospeter Muhongo (PhD - Geology), wazalendo hao ni wadau wetu muhimu katika Mtandao wa Wanaataluma Tanzania.
Pia na tunamshukuru na Mhe. Rais kwa kumteua Mhe. James Mbatia Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi kuwa Mbunge, Mhe. Mbatia ni msomi mzuri sana, mwanaharakati  na Mzalendo wa kweli kwa Taifa letu .

Uteuzi wa wanataaluma hawa unadhihirisha ukweli kuwa Mhe. Rais ana nia njema ya kujenga umoja wa kitaifa na kutumia baadhi ya vipaji tulivyonavyo katika kuleta suluhisho za baadhi ya changamoto tunazokabiliana nazo kwa sasa.
Pia inatukumbusha kuwa unapokuwa  na taaluma fulani basi ni vizuri ukaitumia kwa faida ya jamii inayokuzunguka kwa ujumla na sio kwa faida yako binafsi. Janet, James na Sospeter wote wamekuwa wakishirikiana vizuri sana na jamii na kila wanachofanya wanaweka Uzalendo na Utaifa kwanza.

Nawapongeza wote walioteuliwa na ni matumaini yangu kuwa watatumia vizuri nafasi hizo kwa kutumia taaluma zao na uzoefu wao katika njanja mbali mbali  na kutoa mchango wa katika kuleta maendeleo ya kweli na ya haraka kwa watanzania.

Kama Miaka 30 iliyopita nchi kama Singapore, Korea ya Kusini , Malaysia n.k zilikuwa na uchumi unaolingana na wetu au chini yetu , Je ni kwa nini leo hii wao wameendelea kwa kasi kubwa na sisi bado tunajikongaja ?

Swali hili kila mtu anahitaji kujiuliza na kuona jinsi gani asasa tutabaidilika kifikra, mawazo na kimatendo ili kila mmoja wetu katika eneo lake achukue hatua zitakazochangia kuleta maendeleo ya haraka kwa jamii yetu.

Baadhi ya mambo ambayo kwa mtizamo wangu mimi yanahitaji kupewa kipaumbele ili yasaidie kutufikisha kwenye Tanzania tunayoitaka ni:
1.       Kuwa wazalendo wa kweli
2.       Kuwa na Maadili na kuzingatia miiko ya taaluma husika
3.       Kuzingatia misingi ya Uongozi/utawala bora
4.       Uwekezaji sahihi katika Elimu
5.       Matumizi sahihi ya rasilimali zetu

Mungu awabariki wote, Mungu ibariki Tanzania.

Nawatakia kila la heri,

Phares Magesa,
Rais- Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN),

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa