Home » » Rais Jakaya Kikwete Amteua Bi Mwanahamisi Omari Kitogo Kuwa Msaidizi Wa Rais,Huduma Za Jamii

Rais Jakaya Kikwete Amteua Bi Mwanahamisi Omari Kitogo Kuwa Msaidizi Wa Rais,Huduma Za Jamii


Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemteua BIBI MWANAHAMISI OMARI KITOGO kuwa MSAIDIZI WA RAIS, HUDUMA ZA
JAMII.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y.
Sefue leo, Jumanne, Mei 8, 2012, mjini Dar es Salaam inasema kuwa
uteuzi huo umeanza Mei Mosi, mwaka huu, 2012.

Kabla
ya uteuzi wake, Bibi Mwanahamisi Omari Kitogo alikuwa Mkadiriaji
Ujenzi Msaidizi (Assistant Quantity Surveyor) katika Kampuni ya COWI,
Tanzania.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
8 Mei, 2012

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa