Home » » SUALA LA AFYA YA UZAZI SALAMA LIPEWE KIPAUMBELE MCHAKATO WA KATIBA MPYA

SUALA LA AFYA YA UZAZI SALAMA LIPEWE KIPAUMBELE MCHAKATO WA KATIBA MPYA


Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA Mwanasheria Tike Mwampipile akizungumza na washiriki wa semina ya mapendekezo ya
kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa maoni ya kuandikwa kwa Katiba Mpya iliyomalizika jana kwenye ukubi wa hoteli ya Blue Pear Ubungo Plaza jijini Dar es salaam.
 
NA MAGRETH KINABO- MAELEZO

JAMII iimeshauriwa kulipa kipaumbele suala ya mapendekezo ya
kuwepo kwa   sheria ya Afya ya Uzazi Salama  katika mchakato wa kuwepo kwa Katiba Mpya ,
ambayo itawezesha watumishi wa afya ambao watasababisha vifo vya wakinamama
wajawazito  au watoto wachanga kwa sababu
za uzembe.
Kauli hiyo
iliyoilitolewa (jana) na Mkurugenzi wa Mtendaji  wa Chama cha Wanasheria Wanawake
Tanzania(TAWLA), Tike Mwampipile,   wakati  akifafanua ya mapendekezo  hayo
iliyoandaliwa  na chama hicho kwa

waandishi wa habari kwenye semina ya siku mbili iliyofanyika , Ubungo Plaza jijiini
Dares Salaam.Semina ya mafunzo hayo  ambayo iliyoanza jana  (juzi) na kumalizika leo(jana)

“ Wito wangu katika jamii ni ni ina wajikubu mkubwa wa kujua
haki zao za msingi na kufahamu wapi pa kuzipata. Afya ya Uzazi Salama ni kitu
muhimu ambacho hakijangaliwa kwa umakini. Hivyo katika mchakato wa Katiba Mpya
suala hili liangaliwe kwa uzito kwa  na
upana wake kujali mama ambaye analemta mtoto hapa duniani  ambaye anaweza kuwa na  Rais au Waziri Mkuu wa kesho,” alisema   Mwampipile.

 Aliongeza kuwa kuwepo
kwa sheria hiyo kutasaidia kupunguza
idadi ya vifo vya wakinamama wajawazitio na watoto wachanga.

Kwa upande wake mtoa mada wa mapendekezo hayo,  Bernadetha Mkandya ambaye pia ni mjumbe wa
bodi ya TAWLA na Wakili wa Kujitegemea alisema  kuwa mwanamke ana haki ya   kuishi na kulindwa ,hivyo sheria hiyo
italuiwezesha taifa kupata watoto waliolelewa katika mazingira bora na afya
njema.   .

“ Tunataka tuwe na sheria ya iyatomlinda mwanamke wakati wa
ujauzito na siku 42 baada ya kujifungua,”  ikiwepo kupanga idadi ya watoto atakaoweza
kuwalea na muda wa kupata mtoto mmoja baada ya mwingine alisema.  
 Akifafanua zaidi
kuhusu sheria hiyo alisema  itamwezesha
mamamjamzito kupata huduma za afya ya uzazi salama bora na ambazo zitamwezesha
kupata vifaa tiba vinavyotakiwa bila gharama yeyote.

Aidha Mkandya aliongeza katika sheria hiyo wamapendekeza
kuwa umri wa uti mzima uwe ni miaka 18 ili kuwezesha mtoto wa kike kuolewa
katika umri unaotakiwa hatua ambayo itasaidia kupunguza athari za afya ya uzazi
 zinazotokana na umri mdogo. Alisisitiza kuwa
ni muhimu kwa makundi yote katika jamii kushiriki katika kutoa maoni ya
mchakato huo.

Mkandya aliongeza kuwa mapendekezo hayo  hayo yanaelekeza kuwepo kwa sheria ambayo
itamwezesha mama mjamzito kusitisha ujauzito pale itakapogundulika kuwa
unasabbaisha athari za kiafya kwa ruhusa ya daktari na ridhaa yake  au endapo atakuwa amebakwa na  kwa ridhaa yake kuwa hana uwezo wa kuendelea
hudumia ujauzito huo na kumlea mtoto  pale atakapojifungua.
Pia ridhaa hiyo inaweza kutolewa na ndugu zake endapo mama
huyo ni mlemavu wa akili .

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa