Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » WAFANYAKAZI WAKUMBUSHWA KUHESHIMU SHERIA NA MIONGOZO YA SERIKALI KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI SINGIDA.

WAFANYAKAZI WAKUMBUSHWA KUHESHIMU SHERIA NA MIONGOZO YA SERIKALI KATIKA SHEREHE ZA MEI MOSI SINGIDA.




Maandamano ya wafanyakazi mkoa wa Singida yaliyofanyika Manyoni mjini kushrehekea sikuu kuu ya Mei mosi.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (wa pili kulia) akishiriki kuimba wimbo wa muungano wa wafanyakazi wakati wa kusherehekea mesi mosi.Wa kwanza kulia ni katibu wa TUICO mkoa wa Singida,Happiness Nshange.Wa kwanza kushoto ni katibu tawala mkoa wa Singida,Liana Hassan na anayefuatia ni kaimu mkuu wa wilaya ya Manyoni,Grace Mesaki. 
Katibu wa mkoa TUICO Happines Nshange akitoa taarifa yake ya shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania TUCTA) mkoa wa Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone akihutubia wafanyakazi na wananchi wa mkoa wa Singida (hawapo kwenye picha) wakati wa kusherehekea siku kuu ya Mei mosi kimkoa zilizofanyika Manyoni mjini.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akimkabidhi sista Lucia Siprian ambaye ni mkuu wa shule ya sekondari ya Amani mjini Manyoni zawadi ya hundi ya shilingi laki nane, laptop moja, fulana 29 baada ya kuibuka mfanyakazi bora katika shule hiyo.Pia alikabidhiwa cheti cha shule hiyo kwa kufanya vizuri kwenye taaluma.
Baadhi ya wafanyakazi waliohudhuria kilele cha sherehe za siku kuu za mei mosi zilizofanyika mjini Manyoni wakionyesha bango lao.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu
Serikali ya mkoa wa Singida,imewataka wafanyakazi kupitia vyama vya wafanyakazi,kuwa mstari wa mbele katika kukemea tabia ya kutoheshimu sheria  na miongozo ya serikali yenye lengo la kudumisha amani na utulivu
Wito huo umetolewa leo (jana 01/5/2012)  na mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone, wakati akizungumza kwenye kilele cha sikukuu ya mei mosi zilizofanyika kimkoa wilayani Manyoni.
Alisema amani na utulivu, ni mambo muhimu sana kwa ustawi wa wafanyakazi na wananchi  kwa ujumla.Bila amani na utulivu,nchi haitakalika,wafanyakazi hawatafanya kazi zao ipasavyo na pia, wao na wananchi  hawatapata fursa ya kujiletea maendeleo endelevu.
 “Niwaombe kila mmoja wetu aendelee kuwa mdau wa amani na utulivu katika mkoa wetu wa Singida.Tuepukane na wale ambao wao wanafikiri haki na amani,vyote vinapatikana kwa maandamano yanayoendana na fujo,ghasia na vurugu”,alifafanua mkuu huyo wa mkoa.
Awali katibu wa TUICO,Happiness Nshange, katika risala yake, alisema watumishi wengi wa kada za chini,hawapati marupurupu hata kama wanastahili malipo hasa yale ya baada ya kufanya kazi za ziada.
Kuhusu sekta ya elimu na afya,alisema “Sisi viongozi wa TUCTA mkoa, tunaunga mkono juhudi za serikali yetu ya mkoa wa Singida,  katika kutilia maanani msukumo wa elimu kuanzia shule za msingi,sekondari na vyuo pamoja na changamoto zilizopo za watumishi wa sekta hiyo.
Kuhusu sekta ya afya,Nshange alisema wanaendelea kuupongeza uongozi wa mkoa wa Singida kwa kuboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya zahanati,hospitali ya rufaa ,ya mkoa na zile zinazoendelea kujengwa
Kwa hisani ya Mo Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa