Home » » JAMBO LEO WAPATWA NA PIGO NA KIFO CHA WILLY EDWARD ALIYE KUWA MHARIRI MKUU

JAMBO LEO WAPATWA NA PIGO NA KIFO CHA WILLY EDWARD ALIYE KUWA MHARIRI MKUU


Mjane wa Marehemu Willy Edward  akiwa kwenye majonzi mazito  katika msiba wa mumewe aliyekuwa  Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili
wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea
kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa
mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni mazishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu,
mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa
baadaye.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida
la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo,
Benny Kisaka (wa pili kushoto) wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa
Jambo Leo, marehemu Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu
Mburahati, Dar es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini
Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa. Kutoka
kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na Julius Rabach.



0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa