Maneno Selanyika na Mariam Ayubu, Dar es Salaam
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa, amesema ndoa zinavunjika kutokana na kukithiri kwa vitendo viovu.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati akizungumza kwenye Tamasha la Kimataifa la Love Tanzania.
Alisema ndoa nyingi zinavunjika kutokana na watu wengi kutomjua na kumshirikisha Mungu katika kipindi cha sherehe zao, hivyo kumkaribisha shetani katika maisha yao yote.
“Wanandoa wanasherehekea tu pasipo kuwa na Mungu ndani yao, si kwa wazee tu bali hata kwa vijana hilo ni tatizo, ikumbukwe kuwa ndoa zinapovunjika wanaoathirika zaidi ni watoto na kuwafanya kuwa katika mazingira magumu,” alisema Askofu Malasusa.
Akizungumzia tamasha hilo, alisema linatarajiwa kushirikisha wahubiri wa kimataifa akiwapo Anderw Palau, aliyealikwa na viongozi wa makanisa kuendesha tamasha hilo, litakaloshirikisha waumini wa dini zote.
“Tunatoa wito kwa watu wengi kujitokeza katika tamasha hili, kwa sababu hapa tunazungumzia Watanzania na si Wakristo wala Waislamu.
“Tamasha hili lina malengo makuu mawili, kwanza kuwafikia watu kwa ujumbe wa amani, upendo na habari njema kutoka kwa Mungu, pia kumuabudu na kumshangilia kwa muda wa miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
“Kumjua Mungu ni jambo muhimu kwetu, kwa kuwa machafuko yanayotokea ya kila mara na ajali za mara kwa mara, tukiwa na Mungu atatusaidia kuimarisha imani zetu na kuwa na maadili mema,’’ alisema Askofu Malasusa.
Alisema katika tamasha hilo kutakuwa na matukio mbalimbali yatakayokua yakitolewa kwa jamii, pia wageni kutoka nchi mbalimbali ikiwamo Uingereza, Marekani, Rwanda na Uganda watakuwapo kushiriki kutoa huduma hizo za kijamii, ikiwamo upimaji wa macho na kugawa miwani yasiyopungua 1,000 katika vituo vinne vya Dar es Salaam.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment