Mama Maria akimkabidhia funguo za trekta moja kati ya kumi
aliyokabidhi, mmoja wa wakulima hao Sheikh Hamis Haji ambaye pia ni
Sheikh wa Kata ya Kwadelo.
Mkazi
wa kijiji cha Kwadelo, Maulid Msema akipokea funguo moja kati ya 10 za
Matrekta yaliyokabidhiwa na Mama Maria Nyerere kwa ajili ya wakulima wa
kijiji hicho kilichopo wilayani
Kondoa, kwa ajili ya kuendeleza shughuli za kilimo kijijini hapo,
katika hafla iliyofanyika Msasani jijini Dar es Salaam jana. Kushoto
anayeshuhudia ni Diwani wa Kata ya Kwadelo, Omari Kariati.
Kisha Kariati akamkabidhi zawadi ya Kitenge Mama Nyerere kama shukurani
ya wananchi wa Kwadelo kujengewa kisima cha maji na baba wa Taifa
Mwalimu mwaka 1961 ambacho hadi sasa kipo.
Halafu akamkabidhi mkoba wa safari kama akitaka kwenda Butiama
Kariati akizungumza neno la kufungua shughuli. Kulia ni Mama Nyerere
Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Maria Nyerere, akimkaribisha,
diwani wa Kata ya Kwadelo, wilaya ya KLondoa mkoa wa Dodoma, Alhaj Omar
Kariati, wakati diwani huyo na ujumbe wake wa wakulima kumi, walipofika
nyumbani kwa Mama Nyerere kwa ajili ya kukabidhiwa trekta kumi kwa
wakulima hao, katika sherehe iliyofanyika nyumbani kwa Mama Maria
Nyerere, Msasani jijini Dar es Salaam, jana.
0 comments:
Post a Comment