Sebastian Mparazo, Dar es Salaam
WATU watatu wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti jijini Dar es Salaam, likiwamo tukio la maiti ya mtoto wa kiume kukutwa ikielea katika kisima cha maji.
Katika tukio la kwanza, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema mtoto huyo wa kiume aliyeokotwa ni mkazi wa Ubungo Kibangu na alitambuliwa kwa jina la Wilbroad Mwamkulu (2).
Katika tukio hilo, alisema mama yake marehemu aliyefahamika kwa jina la Tansila Andrea (27), aligundua kuwa mtoto wake amefariki baada ya kumtafuta bila mafanikio.
“Inasemekana huyo mama alipoamka asubuhi hakumuona mwanaye na alipoanza kumtafuta mwishowe alimkuta kwenye kisima cha maji kilicho jirani na nyumbani kwao,” alisema Kenyela.
Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na upelelezi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Katika tukio la pili, alisema lilitokea katika makutano ya Barabara ya Bagamoyo eneo la Africana, ambapo mtu mmoja alifariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari.
Kamanda Kenyela alisema ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T 767 CAM, aina ya Scania ambalo lilikuwa likiendeshwa na Mbwana Said (39), mkazi wa Kitunda na kwamba gari hilo liligonga pikipiki yenye namba za usajili T 62 BTL.
Alisema mwendesha pikipiki huyo aliyetambuliwa kwa jina la Rashid Mnzavas (46), alikuwa akitokea Goba na kwamba aligongwa baada ya kuingia katika barabara kuu bila tahadhari.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala na jitihada za kumtafuta dereva wa gari ambaye alikimbia baada ya ajali hiyo, zinaendelea.
Katika tukio jingine, alisema katika makutano ya Barabara ya Uhuru, eneo la Gapco, mwanafunzi mmoja amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T 287 ADR, aina ya Scania lililokuwa likiendeshwa na Ali Ramadhan (34), mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam.
Alisema gari hilo lilikuwa likitokea buguruni kuelekea karume, ambapo lilimgonga mwanafunzi aliyekuwa akitembea kwa miguu aliyetambulika kwa jina la Abulkarim Mohamed (11) anayesoma darasa la nne, Shule ya Msingi Boma. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment