Mkurugenzi  wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania TTB Dk Aloyce Nzuki wa tatu kutoka  kushoto akiwa katika picha ya pamoja na watanzania hao wakiwa wameshika  vyeti vyao  kushoto ni Wilfred Moshi, Respicius Baitwa wa pili kutoka  kulia na Juma K. Nugaz aka Antonio Nugaz wa tatu kutoka kushoto  wengine  ni Geofrey Meena Meneja Masoko wa TTB na Devotha Mdachi Mkurugenzi wa  Masoko wa pili kutoka kushoto.
Bodi  ya Utalii Tanzania TTB leo imetoa vyeti kwa watanzania watatu  walioipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masuala ya Utalii.
Mkurugenzi  wa Bodi ya Utalii nchini Tanzania Dk Aloyce Nzuki Akizungumza na  waandishi wa habari kwa  ajili ya tukio muhimu la kuwatunikia vyeti  watanzania wa tatu  amesema watanzania hao waliweza kupeperusha bendera  ya Tanzania vizuri hasa katika masuala ya utalii, kwa hapa Tanzania na  nchi za nje.
Watanzania  hawa wameweza kufanya mambo makubwa ambayo kwa kiasi kikubwa sana  yamechangia kwenye sekta ya utalii.Watanzania ambao tunaowapa tuzo leo  ni pamoja na
- Mr. Respicias H. Baitwa
 - Mr. Wilfred Moshi
 - Mr. Juma K. Nugaz
 
1.    Mr. Respicius BaitwaNi mtanzania wa kwanza ambaye ameweka rekodi ya  Afrika kwa mwafrika wa kwanza anatarajia kupanda vilele saba virefu  katika mabara yalioko duniani. Mr. Baitwa mpaka sasa ameshapanda vilele  4. Ameshapanda kilele cha kwanza Mt. Kilimanjaro zaidi ya mara 100,  amepanda Elbrus kilele kirefu katika nchi za ulaya, Aconcagua, Argentina  na Kosciusko Australia.
- 2. Mr. Wilfred Moshi
 
Wilfred  Moshi amekuwa mtanzania wa kwanza kupanda kilele kirefu kuliko vyote  duniani kilele cha mlima Everest. Wilifred Mosha alipanda mlima Everest  mwezi may 2012 na amekua mwafrika wa 3 kupanda na kufika kilele cha  mlima Everest, na kupandisha bendera ya Tanzania kwa kufanya hivyo  Wilifred Mosha ameweza kutangaza jina la Tanzania na kwenye mahojiano  mbalimbali na vyombo vya habari duniani ameweza kutangaza vivutio vya  utalii wa Tanzania kwa ujumla wake.
 3.   Mr. Juma K. Nugaz (Antonio Nugaz)
Juma  Nugaz mtayarishaji wa kipindi cha utalii cha Kambi Popote kinachorushwa  na clouds TV amekuwa mtangazaji bora katika kuhakikisha utalii wa ndani  kwa mwaka 2012 tuzo iliytolewa na chama cha waandishi wa habari  Tanzania.
Mr.  Juma Nugaz amekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utalii wa ndani  kupitia kipindi cha kambi popote na amekuwa akitembelea bila kuchoka  vivutio vya utalii na mwaka jana mwezi wa Disemba aliweza kurekodi  kipindi maalum wakati wa zoezi la kupanda mlima kwa baadhi ya watanzania  katika sherehe za kuazimisha miaka hamsimi (50) wa Tanzania bara ya  Uhuru.Tunampongeza sana.
  Bodi ya utalii Tanzania inawapongeza watanzania hawa kwa kufanya juhudi  kubwa ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii wa Tanzania na tutaendea  kushirikiana nao kutangaza vivutio vyetu zaidi.
Pamoja  na kuwazawadia cheti hiki vilevile tunawazawadia safari ya kitalii  kwenda mbuga za wanyama za Selous kwa siku nne na familia zao.
Chanzo: Father kidevu 
0 comments:
Post a Comment