na Happiness Mnale
WANANCHI wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, Dar es Salaam watakosa umeme siku nzima kutokana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kufunga transfoma mpya yenye saizi ya 15MVA katika kituo cha umeme Mbezi.
Taarifa iliyotolewa na TANESCO imeeleza kuwa, wananchi hao watakosa umeme siku ya Jumamosi, kuanzia saa mbili asubuhi hadi 12 jioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo maeneo yatakayokosa umeme ni Mbezi Tangi bovu, Mbezi Lyagunga, Mbezi Zawadi, Shoko, Mwenge Survey, Mwenge stendi, maeneo ya Jeshi na Hospitali ya Lugalo.
Maeneo mengine ni Kawe, NBC Kawe, 2000 Industries Ltd, Majembe Auction Mart Mwenge na maeneo ya jirani, Mbezi bondeni, Luvent Street, Almas Street, Mwl. Nyerere School, Mbezi Maguruwe, barabara za simba, Chui, Aly Sykes, Beach, BoT Mbezi na TTCL Mbezi Beach.
Pia maeneo ya Zena Kawawa, Roman Catholic Mbezi Beach, Mbezi miti mirefu, uwanja wa walenga shabaha, Jangwani Beach, Belinda na Giraffe, Whitesands na Green Manner hotels, Kilongawima, NMC quarters, Mbezi Juu, Mbezi Samaki, Baraza la Mitihani Mbezi, shule za St. Marys, Mbezi Garden, Ndumbwi, Mbezi kwa Msomali na Mbezi Makonde.
Vile vile katizo hilo pia litaathiri maeneo ya Mbezi Machakani, Mbezi NSSF, ghorofa za Mbezi Masoko ya Kariakoo, Mbezi Jogoo, Art Garlery, Agape Television, Maaza Juice Factory, Kiwanda cha Polypet, Interchik, Kiwanda cha Chemi & Cotex na maeneo ya jirani.
Taarifa hiyo ilitoa tahadhari kwa wananchi kutokushika waya uliokatika, pia imewaomba radhi wananchi kwa usumbufu huo.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment