na Mwandishi wetu
MASHINDANO ya kuwasaka warembo wa utalii mwaka huu, Miss Utalii Ilala na Miss Utalii Kinondoni, yanatarajiwa kurindima jukwaa moja ndani ya Hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation – Dar es Salaam, Yelemia Mayenga, alisema Miss Utalii Ilala na Kinondoni 2012, watawasha moto kwa pamoja, ambako keshokutwa itakuwa shughuli pevu ya kuoneshana vipaji kwa warembo, kabla ya fainali yenyewe, Septemba 14, katika hoteli hiyo.
“Shindano hilo litatanguliwa na la vipaji litakalofanyika Septemba 7 kuanzia saa mbili usiku hapo hapo Lamada Hotel, kiingilio VIP ni sh 20,000 na kawaida ni sh 10,000, na kufuatiwa na fainali Septemba 14, ambako kiingilio kitakuwa VIP sh 30,000 na na sh 10,000 viti vya kawaida,” alisema Mayenga.
Kwa upande wa burudani, mkurugenzi huyo alibainisha kuwa kutakuwa na ngoma za asili, bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ na T Moto Taarab.
Wadhamini wa shindano hilo ni Lamada Hotel, Rashid Sports Entertainments, Mzee Yusuph Enterprises, Zizzu Fashion, Essy Media, Pandisha Import, Tambaza Court Broker and Action Mart, Dar es Salaam City Collage, Geita Gold Mine Limited, Travertine Hotel, Eriado Point View, Stamford Bridge Institute of Journalism, Community Development and Business Studies.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment