Home » » Rafiki Elimu Foundation Wazindua Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini Na Vijijini " EUMIVI PROJECT "

Rafiki Elimu Foundation Wazindua Mradi Wa Elimu Ya Ujasiriamali Mijini Na Vijijini " EUMIVI PROJECT "






Wajasiriamali
wakifanya  "  practical "  ya  kutengeneza  sabuni  ya  maji  kwa 
vitendo  mara  baada  ya  kupokea  maelekezo  kutoka  kwa  waalimu  wa 
ujasiriamali  kutoka  katika  Asasi  ya  RafikiElimu   Foundation. 
Mwanafunzi
wa  ujasiriamali  akitengeneza  sabuni  ya  unga  mwenyewe  mara 
baada  ya  kupata  maelekezo  kutoka  kwa   waalimu  wa  ujasiriamali 
kutoka  RafikiELIMU  Foundation.
Mwalimu
wa  Ujasiriamali  kutoka  katika  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation,
Mama  Ashankira  Lupembe  , akifundisha  kwa  vitendo  namna  ya 
kutengeneza  sabuni   ya  maji.
Baadhi
ya  wajasiriamali  walio  hudhuria  katika   Uzinduzi  wa Mradi  wa 
Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  uliofanyika   leo 
jijini  Dar  Es  salaam. 




Akiulezea
mradi huu, mratibu msaidizi wa mradi huo alisema kuwa mradi huu upo
katika awamu kuu mbili. Awamu ya kwanza itafanyika kuanzia tarehe 01
Septemba 2012 hadi tarehe 29 Septemba 2012, na utafanyika katika mikoa
ya Dar Es salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Morogoro, Dodoma na
Kilimanjaro, ambapo mbali na kutoa mafunzo ya ujasiriamali, asasi
itatafuta vijana kumi na wawili kutoka katika hiyo mikoa saba kwa ajili
ya kufanya kazi kama wajitoleaji " volunteers" katika awamu ya pili ya
mradi itakayo anza rasmi tarehe 01 Novemba 2012 na kuchukua miaka miwili
hadi Novemba 2014 ambapo ndipo itakapo kuwa tamati ya mradi huu.




Awamu
ya kwanza ya mradi huu inafanyika katika mikoa ya Dar Es salaam,
Arusha, Morogoro, Kilimanjaro, Dodoma, Mwanza na Mbeya. Jijini Dar Es
salaam, mafunzo yanafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 01 Septemba
2012 hadi tarehe 04 Septemba 2012 katika Shule ya Msingi Mlimani ,
iliyopo katika Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam... Ratiba kamili ya awamu ya
kwanza ya mafunzo haya ni kama ifuatavyo :




1.
ARUSHA, MOSHI & MOROGORO : Mafunzo yatafanyika kuanzia tarehe 17
hadi 19 Septemba 2012.. Mwisho wa kujiandikisha katika " programme hii "
kwa wakaazi wa ARUSHA, MOSHI na MOROGORO ni tarehe 15 Septemba 2012.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa