Nyumba iliyounganishwa umeme kwa njia ya wizi.
Fundi akiondoa mita ya wizi kwenye nyumba hiyo.
Nyaya zilizokutwa ndani ya nyumba ya mtu mmoja ambaye alikua anaunganishiwa umeme na wezi hao.
Wahandisi wa shirika hilo wakiangalia baadhi ya nguzo zilizokatwa na wezi hao.
Gari liking’oa nguzo hizo za wizi.
Wakiangalia nyaya zilizokatwa na kuibwa kwenye nguzo na kuwakosesha wengine umeme.
Meneja wa Tanesco Kanda Temeke Richard Mallamia, akionyesha namna umeme ulivyounganishwa kimakosa na wizi huko Toangoma.
Na Said Powa.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Shirika la umeme Tanzania (Tanesco) Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam limegundua wizi wa aina yake baada ya kukamata nguzo zaidi ya 6 na nyayazake zaidi ya mita 600 zilizosambaziwa umeme mitaani na wezi kwa kushirikiana na wenye nyumba.
Akizungumzia tukio hilo mbele ya waandishi wahabari wakati wa operesheni hiyo iliyofanywa kwenye eneo la Toangoma Kigamboni Meneja wa Tanesco Kanda ya Temeke Mhandisi Richard Mallamia, amesema wamepenyezewa taarifa za wizi huo na raia wema na tayari kabla ya kufika kwenye operesheni hiyo uchunguzi wa awali unaonyesha kuna uwezekano wa watendaji wa shirika kuhusika na tukio hilo.
Aidha kwenye zoezi hilo ambalo lilikuwa kama la kushitukiza kwenye eneo la Toangoma Masaki mmiliki wa nyumba moja ambayo walikutwa mafundi wakiendelea na ujenzi aliunganisha umeme kwa kushirikiana na wezi hao kwa kujichomekea nguzo zake mbili hadi kufikia nyumba yake ikiwa ni umbali wa zaidi ya mita 200 bila ya kufuata taratibu za shirika.
Akielezea tukio hilo Mhandisi wa Mkoa huo Ebenezer Fue, amesema pamoja na kutofutwa kwa taratibu za uunganishaji lakini pia uunganishwaji wake ni wahatari kwa kuwa haujazingatia viwango vya kitaalamu.
“Hivi vifaa vyote ni vya shirika lakini vimefikaje huku na nani amevileta huku, ndio hatua hii tuliyoanza kuchukua sasa itabainisha, ingawa tumeanza kutajiwa majina ya baadhi ya wahusika wa kazi hii ambao wamo ndani ya shirika lakini ni mapema sana kuwataja kwa sasa ngoja tuendelee na kukusanya taarifa zaidi” Mhandisi Malamia alifafanua.
Kwa mfumo huohuo operesheni hiyo ilibaini maeneo mengine mawili kwenye kitongoji hicho cha Toangoma ambako pia zimechomekwa nguzo nne zikiwa na nyaya zake huku wateja hao wakisubiri hatua za mwisho kuingiziwa umeme ndani ya nyumba zao wakati shirika hilo likiwa halina taarifa za wateja hao.
Katika uchunguzi huo wa Tanesco jambo la kusikitisha linalohujumu shirika ni kuwa wezi hao wamekuwa wakikata nyaya kwa wateja waliounganishiwa umeme kihalali kwenye mitaa na kuchukua nyaya zao kwa lengo la kuwaunganishia watu wengine.
Kwa mujibu wa taratibu za shirika hilo ‘service line’ za umeme zote zinakuwa tayari kwenye ramani ya eneo la kusambazia umeme lakini wateja walikutwa na umeme huo bila kufika kwenye ramani ya eneo husika.
Hata hivyo Mhandisi Mallamia alisema wizi huo umelisababishia hasara shirika kutokana na nguzo zilizotumika kusambaza umeme sio nguzo halali.
Aidha Mallamia amewapongeza wananchi wenye uchungu na shirika lao kwa kutoa taarifa za wizi huo na kuwataka kufanya hivyo mara kwa mara ili kufichua uovu.
Chanzo Mo Blog
0 comments:
Post a Comment