Na Onesmo Kapinga, Dar es Salaam
CHAMA cha Soka Wilaya ya Temeke (TEFA), kimetoa siku tatu kwa Salum Mkemi kukiomba radhi chama hicho, kutokana na kauli yake inayolenga kuleta mgogoro.
Mkemi, ambaye ameenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), katika uchaguzi wa Mkoa huo, kutokana na kukosa sifa, alisema vyama vya soka vya wilaya vya Temeke, Ilala na Kinondoni havina uhusiano mzuri na DRFA.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa TEFA, Mustapha Kassim, alisema madai ya Mkemi ni hatari na yana lengo la kupandikiza mgogoro kwa malengo yake binafsi.
Kassim alisema kwa miaka nane Dar es Salaam, hakuna mgogoro kutokana na ushirikiano mzuri wanaoupata kutoka kwa uongozi wa DRFA unaomaliza muda wake.
Alisema wamekuwa wakipata ushirikiano mzuri kutoka kwa DRFA, hasa katika suala la uandaaji wa Ligi ya wilaya na Kanda ya mkoa huo.
Kassim alisema TEFA imekuwa ikipata ushauri kutoka DRFA na mara nyingi wamekuwa wakisaidiwa fedha kwa ajili ya uendeshaji ya ligi yao.
Alisema Februari mwaka huu, chama hicho kilishiriki katika kupitisha mapato na matumizi ya DRFA katika mkutano wake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kassim alisema DRFA kimekuwa kikitoa fedha kwa ajili ya utawala na masuala mengine ya maendeleo ya soka ya Temeke.
Alisema Mkemi asijaribu kuvigombanisha vyama hivyo, kutokana na kipindi cha miaka nane Dar es Salaam imetulia na hakuna mgogoro.
Kassim alisema Mkemi anatakiwa kukiomba radhi ndani ya siku tatu na akishindwa watamchukulia hatua kali za kisheria.
Alisema kauli yake ina dalili zote za kutaka kuvurugu amani na utulivu iliopo katika Mkoa wa Dar es Salaam, ili aweze kuwania nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Kassim alisema mgombea huyo, anatakiwa kufanya hivyo, kupitia chombo cha habari alichotumia kutoa matamshi ya kuwagawa wanachama wa DRFA, kwa kuwa yeye anataka uongozi.
"Mkemi asitumie TEFA kama daraja la kupata uongozi DRFA, tunamfikisha kwenye vyombo vya sheria asipotuomba radhi," alisema Kassim.
Uchaguzi wa DRFA umepangwa kufanyika Oktoba 14, mwaka huu.

Chanzo: Mtanzania
0 comments:
Post a Comment