Home » » Airtel yawazawadia 500% bonus ya Muda wa Maongezi kwa wateja wake

Airtel yawazawadia 500% bonus ya Muda wa Maongezi kwa wateja wake


Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor, (katikati) akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Ofisi z Airtel Morroco jijini Dar es Salaam leo wakati wakitangaza promosheni mpya ya “Jipatie Mara 5” kwa wateja wake wan chi nzima. Kushoto  ni Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Airtlel, Beatrice Singano Malya na kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Cheikh Sarr.
****  ****
Dar es salaam Octoba 2012 Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpya kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima. Promosheni hii ijulikanayo kama “Jipatie Mara 5” itawawezesha wateja wa Airtel kupata MARA TANO  ya wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Airtel tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu nchi nzima mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku promosheni hii ya “Jipatie Mara 5”. 

Promosheni hii itawazawadia wateja wa Airtel mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo , hii ni sawa na asilimia 500 ya bonus.

”Tumefanya hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendeleza kudhibitisha dhamira yetu ya  kuwapatia wateja wetu nchini nzima uhuru wa kuongea  aliongeza Elangalloor .”

Akifafanua juu ya promosheni hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel Beatrice Singano Mallya alisema” kila mteja wa Airtel tayari ameshaunganishwa katika promosheni hii, kinachotakiwa kufanya ni kupiga simu upate bure salio mara 5 ya wastani wa matumizi yako ya siku kadri mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu ndivyo anajipatia  nafasi  zaidi ya kuzawadia asilimia 500 ya bonus ya muda wa maongezi
“Jipatie Mara 5” ni promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya awali, kila mteja atapata ujumbe utakaomjulisha wastani wake kwa siku na kisha kupokea ujumbe mara atakapopokea asilimia 500% kutoka Airtel. Kwa maelezo zaidi juu ya  huduma hii piga 0783001001 bure na kuunganishwa moja kwa moja na taarifa mbalimbali za huduma zetu”aliongeza Mallya.

Airtel inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini.  kwa kupitia huduma ya Airtel money, Airtel imewawezesha watanzania kupata  huduma za kifedha kirahisi  katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa kuthibitisha uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za kifedha Airtel imewawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa chini ya shilling 100,000/= bure bila makato yoyote. Vile vile Airtel imeendelea kupanua zaidi  huduma za internet kwa  kuwezesha miji zaidi ya 30 nchini kupata internet yenye  kasi ya  3.75G .
 Mkurugenzi wa Mahusiano na Mawasiliano wa Airtlel, Beatrice Singano Malya akifafanua jambo kwa waandishi wa Habari, pamoja nae ni Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor
 Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Cheikh Sarr, akitoa maelezo juu ya Promosheni hiyo kwa waandishi wa Habari, pamoja nae ni Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Cheikh Sarr, akitoa maelezo juu ya Promosheni hiyo kwa waandishi wa Habari, pamoja nae ni Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor (kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano, Beatrice Singano Malya.
 Wanahabari wakiwa kazini kupata matuki
Afisa Mahusiano wa Airtel, Dangio Kaniki akigawa vipeperushi vya Promosheni hiyo .

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa