MBUNGE wa Iringa mjini na
Waziri Kivuli wa Mali Asili na Utalii (Chadema) Mch. Peter Msigwa amemtaka rais
Kikwete kuchukua hatua za maksudi na kuingilia kazi za Waziri wa Maliasili na
Utalii kwa madai kuwa waziri huyo ameshindwa kazi na anakula sahani moja na
majangili.
Akiongea na waandishi wa habari
leo jijini Dar es salaam Msigwa amesema anasikitishwa na hatua ya serikali
kukaa kimya ili hali ujangili wa pembe za ndovu ukiendelea huku waziri huo wa
mali asili na utalii Balozi Hamisi Kagasheki akiwa kimya.
Msigwa aliyasema hayo kufuatia kukamatwa kwa pembe za ndovu
huko Hong Kong, China jambo ambalo alitegemea Tanzania wizara husika ungechukua
hatua za haraka kubaini wezi waliosafirisha bidhaa hiyo lakini wizara imekaa
kimya hata baada ya mamlaka za China kuomba taarifa za mtandao wa biashara
hiyo.
“Pembe za ndovu zenye uzito wa
tani 4 kutoka nchini Tanzania na Kenya zimeripotiwa kukamatwa na vyombo vya
usalama vya mamlaka ya jiji la Hong Kong hivi karibuni, huku zile zilizoibwa
kutoka Tanzania zikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5 lakini waziri
hata hashtuki amekaa kimya”
Alisema wizi huo wa pembe za
ndovu ni matokea ya waziri Kagasheki kuendelea kuwalinda watuhumiwa wakuu wa
ujangili na kufanya danganya toto kwa kuwachukulia hatua watuhumiwa watatu tu
wadogo, huku wale vigogo wa ujangili wakiachwa waendeleze ujangili kwa maslahi
anayoyajua yeye na chama chake cha CCM.
“Kuendelea kwa matukio ya
ujangili ni ushahidi kuwa mabadiliko ya Mawaziri yaliyofanywa na Rais Kikwete
kwa kuwatoa Maige na kumweka Kagasheki hayajazaa matunda yoyote, kwani udhaifu
au ufisadi wa Kagasheki hauna tofauti yoyote ile na ule uliosababishwa na
mtangulizi wake aliyeondolewa” alisema Msingwa.
Akitoa msimamo wake juu ya
jambo hilo waziri huyo kivuli wa mali asili na utalii amesema wizara ya
maliasili na utalii ni njia kubwa ya utoroshaji na wizi wa rasilimali za taifa
na kwamba pamoja na mabadiliko ya mawaziri bado ufisadi unaendelea.
“Kwa mara nyingine tena napenda
watanzania wafahamu kwamba uwendawazimu ni kufanya jambo lile lile kwa njia ile
ile huku ukitengemea matokeo tofauti, kwa kadri muda unavyozidi kwenda wanyama
pori na rasilimali nyingi za nchi hii zitaendelea kuibiwa na kuuawa, naomba
rais achukue hatua za maksudi kunusuru hali hii” alisema Msigwa.
Chanzo: tabianchi blog
0 comments:
Post a Comment