Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki mazoezi ya viungo baada ya kumaliza kushiriki na kuhitimisha matembezi ya hisani ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Matembezi hayo yalianzia katika Viwanja vya Karimjee jijini na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal,akimkabidhi cheti, Mhandisi Grace Beo, kutoka Kampuni ya Temesa ICT Engineer, akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Moahammed Gharib Bilal,akimkabidhi cheti, Mhandisi Morgan Nyonyi, kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), akiwa ni mmoja kati ya waliochangia na kushiriki vyema katika zoezi la kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uwezo wa Wahandisi wa Tanzania, yaliyoandaliwa na Wahandisi hao (Local Engineers). Makamu alikabidhi vyeti hivyo baada ya kuhitimisha rasmi matembezi hayo ya hisani yaliyoanzia katika Viwanja vya Karimjee na kumalizikia kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam, leo Oktoba 7, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na Wahandisi (Local Engineers) baada ya kuhitimisha matembezi hayo katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni, jijini Daar es Salaam leo, Oktoba 7, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
========= ====== ========
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewahakikishia wahandisi nchini kuwa serikali inaendelea kuongeza udahili kwenye taaluma muhimu katika vyuo vikuu ili kujenga uwezo wa wahandisi wazalendo.
Dk. Bilal ameyasema hayo leo katika hotuba yake aliyoitoa katika kuhitimisha matembezi ya hisani kuchangisha fedha za kujenga uwezo wa wahandisi Watanzania kwenye viwanja vya Leaders club mjini Dar es salaam.
Alisema katika kufanikisha azma hiyo hivi sasa baadhi ya vyuo vikuu nchini vimeanzisha programu za shahada za uchimbaji madini na mafuta na utengenezaji nguo na pia Serikali imejenga taasisi maalum ya Nelson Mandela ili kukuza kwa kasi zaidi maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini.
“Hivi sasa serikali inatekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya uchimbaji madini, mafuta na gesi. Miradi yote hii ili iweze kulinufaisha taifa inahitaji kuwa na wahandisi wazalendo ambao wako tayari kutumia ujuzi wao kwa maslahi ya Taifa”, alibanisha Makamu wa Rais.
Aliwaambia wahandisi hao kwa Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kuhakikisha maliasili za hapa nchini zinavunwa na kutumiwa kwa manufaa ya Taifa na kukiri kwamba jambo hilo haliwezi kufanikiwa kwa kiwango kinachohitajika iwapo nchi itaendelea kutegemea na kutumia wataalam wengi kutoka nje ya nchi.
Alisema pamoja na kupanua elimu ya vyuo vikuu, Serikali inaendelea kuimarisha taasisi za Manunuzi ya Umma na Usimamizi na Uthibiti wa Kitaalamu ili kuhakikisha kwamba sera, sheria na maslahi ya Watanzania vinazingatiwa ikiwemo upatikanaji wa tija muafaka kwenye miradi na kuongeza fursa za ajira kwa wataalamu wa hapa nchini.
“Lakini lazima tuitakidi kama wataalamu kuwa hakuna litakalotushinda kama tutadhamiria kulifanya. Tujenge misingi ya kukuza weledi, ufanisi, ubunifu na tusimamie maadili ya fani zetu na pamoja ya nchi yetu”, alisema Dk. Bilal
Mapema, akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Taasisi ya Wahandisi Tanzania Mhandisi Dk. Malima Bundara alielezea nia yao ya kutaka kuanzishwa kwa Ofisi ya Mhandisi Mkuu wa Serikali ili iweze kushughulikia masuala ya wahandisi kama ilivyo kwa kada zingine.
Imetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es salaam
Jumapili, Oktoba 7, 2012
0 comments:
Post a Comment