Naibu Waziri Philipho Mulugo
Kuanzia juzi taarifa na video ya Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi wa Tanzania Philipo Augustino Mulugo zimeanza kusambaa kwa watanzania wengi kuhusu alichosema akiwa Afrika Kusini kwenye mkutano wa kimataifa kwamba Tanzania ni muungano wa visiwa vya bahari ya Hindi, Pemba na Zimbabwe.
Mulugo leo amezungumza na Power Breakfast ya CLOUDS FM na kusema kabla ya yeye kupanda kuanza kuzungumza kulikua na kiongozi wa Zimbabwe ambae alitoka kuzungumza na nina mkariri akisema
“sasa ilibidi lazima baada ya kufika pale ni lazima umshukuru mwenzako aliepita sasa kama mawazo ndiyo yaliyokua yamedhania hivyo kwamba basi hapa naitamka Zimbabwe kwa sababu zote zimeanzia na Z labda ilitokea hivyo lakini nakiri kabisa kwamba sikua na makusudio kwamba naitamka Zimbabwe lakini kule kwenye power presentation inaonekana kabisa ukifungua pale ni Tanzania imeungana na Zanzibar Pemba na Tanganyika kama ambavyo tunajua kwa sababu ile ni historia hakuna asiejua hata mtoto wa darasa la tatu”
“Niseme tu kwamba hiyo ni kuteleza kwa ulimi na nilikua namfikiria yule waziri wa Zimbabwe kwa sababu alikua ametoka kuhutubia kabla ya mimi, nilikua naomba ieleweke hivyo…………
na wengi wameongea wanahoji lugha kiingereza, jamani tukubaliane kwamba kusema Zimbabwe badala ya Zanzibar sidhani kama inaendana na drama yenyewe kwa sababu mimi nimekua mwalimu mda mrefu nimefundisha wanafunzi wangu na wananifahamu uwezo wangu mkubwa na tena mimi ni mwalimu wa historia hata degree yangu ni mimi ni mwalimu wa historia na Economics,
labda niliongea nilikua sijielewi na ningegundua nimetamka Zimbabwe ningeweza kuomba radhi, mataifa yote wawe waafrika wawe wazungu wengi huwa tunazingatia kuangalia kwenye power point pale, wengi huwa hawasikilizi sauti” – Mulugo
Kuhusu kukosea kutaja mwaka, Namkariri naibu waziri akisema “mimi pale nia yangu ilikua ni kusoma namba moja moja nikashtukia nakwenda kusoma mbili, haijakaa kama nimekosea kiingereza kama watu wanavyoipanua kwa mfumo huo lakini kama watu wamenielewa hivyo niombe tu msamaha”
0 comments:
Post a Comment