Balozi wa Kampuni ya Glenmorangie Bw. Niel Hendriksz akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili leo hapa nchini akionyesha baadhi vya vinywaji vya kampuni hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine pia anatarajiwa kutoa mafunzo maalum kwa baadhi ya wahudumu kutoka baa kubwa ambayo yatakusa sio tu uchanganyaji sahihi wa wiski za Glenmorangie bali pia historia fupi ya na aina tofauti za Glenmorangie.
Lengo Kuu la mafunzo hayo ni kuwapa wahudumu ujuzi utakaowawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na Glenmorangie kwenye baa au hoteli.
Glenmorangie inafahamika kama kinywaji cha wisk pekee kutoka Scotland (Single Malt Scotch Whiskey) tamu na inayopendwa zaidi duniani.
Balozi wa Glenmorangie Bw. Niel Hendriksz amewasili leo jijini Dar Esa Salaam kwa ziara ya siku mbili ikiwa ni katika ziara yake ya siku 5 katika Ukanda wa Afrika Mashariki.
Katika ziara yake hiyo ya siku mbili nchini, Hendriksz atakutana na wapenzi wa Wisk katika matukio mbalimbali maalum ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Dar Es Salaam Serena ambayo itawapa wapenzi wa Glenmorangie nafasi ya kuonja aina mbali mbali za wiski kutoka Glenmorangie.
Dhimuni la ziara yake ni kuwazawadia wanywaji wa Glenmorangie pamoja na kuwaelimisha na kujenga na kuwapa kujenga uelewa kuhusu utumiaji wa vinywaji vya Glenmorangie katika ukanda wa Afrika Mashariki.
0 comments:
Post a Comment