Home » » Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa India hapa nchini

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa India hapa nchini



Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) (kulia) akisalimiana na Balozi wa India hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw aliyefika ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri kwa lengo la kujitambulisha ambapo pia walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
Mhe. Naibu Waziri (kushoto) akizungumza masuala mbalimbali na Mhe. Balozi Shaw wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha.
Mhe. Balozi Shaw (kushoto) akizungumza  huku  Mhe. Naibu Waziri akimsikiliza kwa makini.
Mhe. Balozi Shaw akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ofisini kwa Mhe. Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri akiendelea na mazungumzo na Mhe. Balozi Shaw. Wengine katika picha ni Bw. Charles Faini (kushoto kwa Mhe. Naibu Waziri), Afisa Mambo ya Nje na Bw. D.K. Pant (kulia kwa Mhe. Balozi) Afisa kutoka Ubalozi wa India hapa nchini.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa