Kansela wa ubalozi wa nchi hiyo Vincent Kalchenko (katikati) akitoa taarifa ya nchi yake kuamua kurejesha nyumbani raia wake aliyejeruhiwa wakati akiogelea katika Pwani ya Kendwa kwa ajili ya matibabu zaidi ya kitaalam. Kulia ni Consul Alexey Loginov na kushoto ni Attaache Nikita Rassokhin.
Na. Mo Blog Team.
Ubalozi wa Urusi nchini umeamua kumsafirisha raia wake Vera Sergeeva kutokana na hali yake ya kiafya kuwa mbaya alipolazwa hospitali ya MI ya jijini Dar es Salaam.
Raia huyo anadaiwa kujeruhiwa na boti kichwani Septemba 23 mwaka huu kwenye pwani ya Kendwa Zanzibar wakati akiogelea.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kansela wa ubalozi wa nchi hiyo Vincent Kalchenko, amesema kuna ulazima wa kufanya hivyo kutokana na hali yake kuwa mbaya zaidi.
Amesema kama ilivyo ada pale raia wa Urusi akipata matatizo nje ya nchi yake, ni jukumu lao kumsaidia kwa njia yoyote ile ikiwemo ya kumtafutia usafiri ukiwemo wa ndege kwa ajili ya kumrejesha nyumbani.
0 comments:
Post a Comment