Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akizindua matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya magonjwa ya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012 uliofanyika leo katika hoteli ya ya Blue Pearl Ubungo plaza jijini Dar es Salaam huku Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa akimuangalia kwa makini. Utafiti huo utatoa viwango vya sasa vya maambukizi ya magonjwa hayo katika kuelezea hali halisi ya sasa ya viashiria ilivyo katika mpango wa MKUKUTA na MKUZA katika Malengo ya Milenia ya 2015.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akimkabidhi Dkt. Jesicca Kafuko kutoka USAID kitabu chenye matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya magonjwa ya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012 ili wakaifanyie kazi . Uzinduzi wa huo uliofanyika leo katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akimkabidhi Khazija Khamis mwakilishi kutoka wizara ya Afya Zanzibar matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012 ili wizara hiyo ikaifanyie kazi. Uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika leo katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiwaonyesha wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa taarifa ya matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya magonjwa ya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012. Hafla hiyo ilifanyika leo katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo plaza jijini Dar es Salaam.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
0 comments:
Post a Comment