Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Mudhihiri Mudhihiri (kushoto) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa shilingi 1,200 kwa daraja la kwanza na 960 kwa daraja la pili. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Masoko wa bodi ya Korosho Tanzania Theofora Nyoni.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Mudhihiri Mudhihiri akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu bei ya mkulima ya kununulia korosho msimu wa 2012/2013 kuwa shilingi 1200 kwa daraja la kwanza na 960 kwa daraja la pili. Ili kumpunguzia mkulima mzigo wa riba ya deni mabenki yatakopesha vyama vya msingi malipo ya awali kwa asilimia 50 badala ya asilimia 70 kama ilivyokuwa kwa msimu wa mwaka jana.
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Mudhihiri Mudhihiri (kulia) akiwaandikia waandishi wa habari jina lake wakati wa mkutano baina yao uliofanyika leo makao makuu ya bodi hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhulia mkutano baina yao na bodi ya korosho uliofanyika leo katika ofisi za bodi hiyo jijini Dar es Salaam wakijitahidi kupata matukio muhimu ya mkutano huo.
(Picha na Anna Nkinda – Maelezo).
0 comments:
Post a Comment