Wasanii wa kundi za sanaa za maigizo la Pamoja
Sanaa Group la mkoani Dar es Salaam kesho wanatarajia kutembelea kituo cha
watoto yatima Mwenge.
Katibu wa kundi hilo Manuary Mruma maarufu kwa
jina la Mr. Nzoke amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kutoa msaada kwa watoto
hao wanaoishi katika mazingira magumu.
Amesema hakuna namna nyingine ya kuonyesha
fadhila za matunda wanayoyapata kutokana na sanaa zaidi ya kwenda kutoa msaada
kwa watu wasiojiweza.
Wasanii hao wakiongozwa na uongozi wa kundi
watafika katika kituo hicho majira ya saa nne asubuhi.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment