Mwalimu Mboya akisindikizwa na walimu wenzake wakitoa msaada wa ndala dazani moja, dawa za mswaki dazani mbili na miswaki dazani mbili. Kuanzia kushoto ni Mwalimu Ana Kimatare, Mzee Hamisi Mwakimwagile (akiyepokea msaada huo kwa niaba ya Tanzania 50 Plus Campaign), Mwalimu Florence Mboya, Mwalimu Happy Lumbwe na Mwalimu Ng’walu Mipawa.
Tanzania 50 Plus Campaign ikishirikiana na waathirika wa saratani na marafiki wa kampeni itatembelea hospitali ya wagonjwa wa saratani katika hospitali ya Ocean Road Cancer Institute tarehe 24 Novemba 2012 saa 4 asubuhi. Ili kufanikisha zoezi hilo imeomba watu binafsi na makampuni mbali mbali na jamii kwa ujumla kuchangia misaada ya sabuni za kufulia, za kuogea, mafuta ya kujipaka (petroleum jelly), miswaki, dawa za miswaki, ndala, maji ya kunywa, juice mbalimbali na mtunda.
Tanzania 50 Plus Campaign inamshukuru sana Mwalimu Florence Mboya kwa ukarimu wake na moyo wa upendo na huruma kwa wale wenye mahtaji. Bado tunaendelea kupokea misaada.
Ukiwa na msaada wako wasiliana nasi:
Simu 0754 402033
au barua pepe: chrptz@yahoo.com,
ekandusi@yahoocom
0 comments:
Post a Comment