Kwa zaidi ya miaka kumi biashara kati ya Africa na ulimwengu kwa ujumla imekua sana, wakati ambapo biashara kati ya Africa na nchi za Gulf Cooperation Council(GCC) imekua kwa asilimia 170.
Mabadiliko yaliyozikumba nchi za Africa kutoka kwenye nchi tegemezi na kuelekea kwenye nchi za kibiashara, na uhusiano uliopo kati ya nchi za Africa na Mashariki ya Kati, imeuweka uchumi unaofuata sheria za kiIslam ktk nafasi muhimu ya kuandaa mazingira ya biashara kati ya Africa na nchi za Mashariki ya Kati.
Umuhimu huo unaongezeka zaidi kwa sababu ya uhusiano mkubwa uliopo kati ya uchumi unaofuta sheria za kiIslam, biashara (real economic activity) na vyanzo vilivyopo ambavyo vinatoa mwanya wa biashara ktk nyanja muhimu kama vile Small and Medium Enterprises (SMEs).
Hamu kubwa ya wajasirimali wa Mashariki ya kati ktk biashara kama za kilimo, kununua ardhi na viwanda, kunategemewa kukuza kwa kiasi kikubwa uchumi wa bara la Africa.
Akizungumza kabla ya kikao mkurugenzi wa Islamic Banking Summit (IBSA) ndugu David McLean alinukuliwa akisema ‘kutokana na mabadiliko ya baadhi ya sheria ktk soko la Africa, Africa imejipanga ktk nafasi ya tatu kwenye orodha ya uchumi unaokua kwa kasi duniani baada ya Mashariki ya Kati na nchi za Asia’.
Alisisitiza kwamba ni kwa sababu kama hizo ndio zimetufanya tukutane kwenye kikao hichi cha the Islamic Banking Summit (IBSA 2012) kama hatua muhimu ambazo zitashughulikia malengo yaliyowekwa na World Islamic Banking Conference (WIBC).
Kikao hicho kinachojulikana kama the Islamic Banking Summit kinategemewa kufanyika nchini Djibouti kwa mda wa siku mbili tarehe 6-7 mwezi wa kumi na moja mwaka 2012 kwa ajili ya kujadili fursa na changamoto zilizopo ktk uchumi huo.
0 comments:
Post a Comment