Home » » Ukaguzi Wa Ujenzi Wodi Za Wagonjwa Wa Fistula CCBRT Wafanyika

Ukaguzi Wa Ujenzi Wodi Za Wagonjwa Wa Fistula CCBRT Wafanyika


  Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya walemavu ya CCBRT, Dr. Wilbroad Peter Slaa akimuonyesha maendeleo ya ujenzi Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za hospitali hiyo kabla ya kukabidhiwa kwa Rais Dk, Jakaya Mrisho Kikwete mapema mwezi huu.
Mkurugenzi wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akiwapiga picha kupitia simu yake ya mkononi watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam wakati alipofanya ukaguzi wa wodi za wagonjwa pamoja na Mabasi ya wagonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhiwa rasmi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr Jakaya Mrisho Kikwete.
 Mkurugenzi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, Dk. Margaret Mhando, akipokea zawadi kutoka kwa moja ya wagonjwa wa Fistula wanaotibiwa katika hospitali ya CCBRT wakati alipofanya ukaguzi wa wodi mpya za wagonjwa wa fistula kabla ya kukabidhiwa kwa Rais. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete. Pamoja nae ni Mkurugenzi  wa Idara ya huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet.
Mkurugenzi  wa kitengo cha huduma za jamii wa Vodafone group, Andrew Dunnet akikagua moja ya mabasi yatakayo tumika kubeba wagonjwa wa Fistula, mabasi hayo yamenunuliwa katika mpango wa kupambana na Fistula uliochini ya CCBRT, Wizara ya Afya na Vodafone uliozinduliwa na Rais Jakaya Kikwete Februali 25.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa