Home » » UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA KUTOKA MTWARA NA SONGOSONGO HADI DAR ES SALAAM

UZINDUZI WA MRADI WA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA GESI ASILIA KUTOKA MTWARA NA SONGOSONGO HADI DAR ES SALAAM




TAARIFA KWA UMMA
Wizara ya Nishati na Madini (MEM)  inapenda kuutangazia umma kuwa Serikali inatarajia kuzindua mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kusafisha na kusafirisha gesi asilia kutoka Mnazi Bay Mtwara na Songo Songo Kilwa  hadi Dar es Salaam.

Hafla ya kuweka Jiwe la Msingi wa mradi huo itafanyika tarehe  8/11/2012 Kinyerezi, Manispaa ya Ilala, katika eneo ambapo mitambo ya kuendeshea mfumo mzima wa gesi itajengwa. Mgeni rasmi katika sherehe hiyo atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Wananchi wote wa Dar es Salaam na maeneo yanayozunguka eneo la Kinyerezi mnaalikwa na mnaombwa kufika kwenye eneo la mradi saa 2.00 asubuhi.

GESI ASILIA KWA MAENDELEO YA TAIFA

Imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa