Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga (wa pili kushoto) akiwasili katika Hotel ya White Sands jijini Dar es Salaam kujionea jinsi Hoteli hiyo iliyopo ufukweni mwa bahari inavyotunza mazingira yake. Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya White Sands Alwyn Kellerman na Afisa Mazingira wa Hoteli hiyo Bi. Linda Mbuya.
Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli hiyo akifunua chemba inayopitisha maji taka kwa ajili ya kukaguliwa na jopo la wataalam kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara. Katika ukaguzi huo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga hakuridhishwa na jinsi hoteli hiyo inavyoendesha mfumo wake wa maji taka na kuagiza timu ya wataalam kutoka NEMC kufanya ukaguzi upya wa mifumo hiyo.
Meneja Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View Bw. Nicholas Oyieko akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Mh. Kitwanga (wa pili kushoto) jinsi hoteli hiyo inavyotunza mazingira na namna inavyodhibit mfumo wake wa maji taka kuhakikisha kwamba haileti madhara.
Hii ni sehemu iliyoko pembeni ya Hoteli ya Giraffe ambayo mmiliki wake hafahamiki ambayo imewekwa uzio na kufanya bahari kushindwa kupumua vizuri na kusababisha mkusanyiko wa uchafu unaodaiwa kutuama mahali hapo tangu mafuriko ya hivi karibuni yaliyoikumba jiji la Dar es Salaam. Naibu Waziri ameamuru muhusika kutafutwa mara moja na kupigwa faini na kuamuriwa kuondoa vifusi hivyo.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga na ujumbe wake wakiangalia eneo hilo.
Mh. Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven Lippinghof baada ya kuwasili hoteli hapo kwa ziara ya kushtukiza kukagua miundo mbinu ya maji taka kwa hoteli zilizopo pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.
Mh. Charles Kitwanga akielekea kufanya ukaguzi wakati wa ziara yake ya kutembelea hoteli mbalimbali za jijini Dar es Salaam zilizopo pembezoni mwa fukwe za bahari ya Hindi.
Wataalamu kutoka NEMC na Maafisa wa Wizara wakikagua moja ya chemba za hoteli hiyo zilizounganishwa na mabomba yanayochuruzisha maji baharini ambapo Hoteli hiyo ilidanganya kwa kusema kwamba kila chemba hizo zinapojaa wanaita gari maalum la kunyonyea maji taka hayo kitu ambacho si kweli kwa mujibu wa watalaam wa NEMC.
Moja ya bomba la maji taka kutoka katika hoteli hiyo yanayotiririkia baharini.
Pichani ni Matundu ya mabomba ya maji machafu yanayotokea Hoteli ya Double Tree By Hilton yaliyoelekezwa baharini.
Naibu Waziri Mh. Charles Kitwanga akitoa amri kwa Mkurugenzi wa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Enviromental Impact Assessment-EIA) wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw.Ignace Mchallo ambapo ametoa muda wa miezi miwili kwa uongozi wa Hoteli ya Double Tree kutafuta njia nyingine ya kumwaga maji taka isiyochafua fukwe na maji ya bahari akisema kuwa yeye si mzungumzaji sana bali anasimamia vitendo. Mheshimiwa Waziri amemtaka Bwana Mchallo kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema watachukua hatua kuanzia kesho (7 Disemba 2012) kwa kuwa Afya za watu hazisubiri muda hivyo tunauwezo wa kumfungia biashara yake, kumlipisha faini au vyote kwa pamoja na tutahakikisha anaacha kumwaga maji taka eneo la baharini.
Mwanasheria wa NEMC Bw. Mwanchane Heche akimpa utaratibu wa mamlaka yake hatua itakayochukua Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Bw. Sven Lippinghof akimweleza kuwa japokuwa huduma zao ni bora mfumo wao wa maji taka unahatarisha Afya za Wananchi na kuharibu Mazingira.
Huu ni muonekano wa Hotel ya Double Tree By Hilton kwa nyuma Upande wa bahari ambako ndiko wateja wao wanakopumzika na kupunga upepo mwanana wa baharini kunakomwagwa maji machafu ya kinyesi.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga ( wa pili kushoto) akizungumza na Meneja Mkuu wa Hoteli ya Coral Beach Hans Heuer (kushoto) ambako alihitimisha ziara yake.
Mh. Charles Kitwanga na Ujumbe wake wakikagua miundo mbinu ya eneo la Coral Beach Hoteli.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mh.Charles Kitwanga akitoa maoni yake kwa Uongozi wa NEMC na kusema kuwa ameridhishwa na hali ya mazingira na utaratibu unaotumiwa na Hoteli hiyo.
0 comments:
Post a Comment