Home » » Mwanamuziki Koffi olomide awasili jijini Dar tayari kwa onesho lake jumamosi

Mwanamuziki Koffi olomide awasili jijini Dar tayari kwa onesho lake jumamosi



Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku huu mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga
Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku huu  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimlaki (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar usiku.Mwanamuziki huyo machachari awapo jukwaani ameshuka na skwadi lake zima la Quartier Latin  kwa ajili ya kutumbuiza siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,ambapo kiingilio kimepangwa kuwa ni  shilingi 10,000/= kwa shilingi 15,000/= getini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akizungumza na (mgeni wake) ,Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide mara baada ya kuwasili kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar usiku huu.
 Baadhi ya wanamuziki wa Koffi Olomide wakishuka kwenye gari kwenye viunga vya hoteli ya Serena usiku huu.
 Baadhi ya wadau na wapenzi waliokumbana uso uso kwa na mwanamuziki Koffi Olomide usiku huu,wakipata picha ya pamoja.
 Mdau Idd Janguo nae alipata picha ya ukumbusho na Koffi Olomide,ambaye anasema amejipanga vyema kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar siku ya jumamosi ndani ya vuwanja vya Lidaz Club.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa