Home » » RAY C Amshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu,ikulu jijini Dar es Salaam

RAY C Amshukuru Rais Kikwete kwa msaada wa matibabu,ikulu jijini Dar es Salaam




Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C akimshukuru Rais Kikwete kwa kumsaidia matibabu,alipomtembelea ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C watu kushoto,Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah Mtweve Dada yake Ray C.Picha na Freddy Maro



Mwanamuziki
wa Kizazi Kipya Rehema Chalamila maarufu kama RAY C leo amemtembelea
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dare s Salaam na kumshukuru
kwa msaada wa matibabu wakati alipokuwa mgonjwa hivi karibuni.

Rehema
aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah
Mtweve alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu
atarejea jukwaani kukonga nyoyo za mashabiki wake.Kwa apande wake ,Mama
Mzazi wa Ray C amemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye na
vilevile ametoa wito kwa watu wanaokusanya michango kwaajili ya mwanaye
waache kufanya hivyo kwani matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa