Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Dar es Salaam
10/12/2012
Serikali inatarajia kuongeza udahili wa wanafunzi wanaosomea masomo katika
sekta ya afya nchini kutoka wanafunzi 7500 hadi 10,000 kwa mwaka ifikapo 2015.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa
wadau wa chanjo barani Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa
Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema udahili huo utasaidia
kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.
Waziri Mwinyi amesema uhaba wa wafanyakazi katika sekta ya afya
umesababisha kutowafikia watoto wote nchini ili kuwapatia chanjo za magonjwa
mbalimbali.
Kwa upande wake muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa
Tanzania, Lufaro Chatora amesema shirika hilo likisaidiana na Wizara ya Afya
wanafanya jitihada ya kuongeza magari ili kuwafikia wototo wote na kuwapatia
chanjo.Mkutano huo wa siku tatu unawakutanisha wadau 200 wa huduma ya chanjo
kutoka nchi mbalimbali barani afrika ambapo pamoja na mambo mengine
watajadili jinsi ya kuboresha na kuimarisha huduma ya chanjo.
0 comments:
Post a Comment