Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com
Home » » UPELELEZI KESI YA MSANII ELIZABETH MICHAEL 'LULU' WAKAMILIKA, KUSOMEWA MASHTAKA DESEMBA 21, 2012

UPELELEZI KESI YA MSANII ELIZABETH MICHAEL 'LULU' WAKAMILIKA, KUSOMEWA MASHTAKA DESEMBA 21, 2012


Na Mwandishi Wetu
MSANII wa filamu hapa nchini, Elizebeth Michael maarufu kwa jina la Lulu, ameanza kuona ahueni baada ya Mahakama ya Mkazi Kisutu, kuelezwa kuwa upelelezi wa kesi ya mauaji didi ya msanii mwenzake, Steven Kanumba, umekamilika.

Kufuatia sakata hilo, Lulu sasa atasomewa shtaka la kuua bila kukusudia badala ya mauaji jalada lake litakapofika katika meza ya Mahakama Kuu.

Wakili wa Serikali, Ofmedy Mtenga alieleza mbele ya Hakimu Mkazi Augustino Mmbando anayeisikiliza kesi ya msanii huyo aliyeacha gumzo katika kuhusishwa na kifo cha Kanumba.

“Mheshimiwa Hakimu, kesi ilikuja kwa ajili ya kutajwa, hivyo upelelezi wake umekamilika na mshitakiwa alitakiwa kusomewa muhtasari, ingawa Wakili wa serikali, Tumaini Kweka hayupo,” alisema Mtenga.

Hata hivyo, Wakili wa mshitakiwa, Peter Kibatala aliiomba mahakama kupanga tarehe ya karibu ili mshitakiwa asomewe muhtasari wa ushahidi dhidi ya mashitaka yanayomkabili.

Hakimu Mmbando alikubali kuahirisha kesi hadi Desemba 21 mwaka huu kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa muhtasari wa ushahidi na kisha jalada la kesi litafungwa, kesi itahamia Mahakama Kuu.

Mawakili wengine wanaomtetea msanii huyo anayetingisha tasnia ya filamu kabla ya kufikwa na maswahibu hayo ni Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe.

Msanii huyo bado yupo rumande kwa miezi nane sasa kutokana na makosa ya mauaji kutokuwa na dhamana, huku akidaiwa kuwa Aprili 7 mwaka huu alimuua Kanumba, maeneo ya Vatican, Sinza, jijini Dar es Salaam.
Kwa hisani ya Habari na matukio Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa