Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Abdallah Zombe
RUFANI ya kesi ya mauaji inayomkabili aliyekuwa
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam (RCO),
Abdallah Zombe na wenzake wanane, inatarajiwa kusikilizwa leo katika
Mahakama ya Rufani.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam (RCO),
Abdallah Zombe na wenzake wanane, inatarajiwa kusikilizwa leo katika
Mahakama ya Rufani.
Hiyo ni baada ya miaka mitatu tangu
ilipofunguliwa na inatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa
Mahakama ya Rufani, linaloundwa na Jaji William Mandia, Jaji Nathalia
Kimaro na Jaji Katherine Oriyo.
Katika kesi hiyo, Zombe na wenzake hao
wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara
watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi wa Manzese,
Dar es Salaam.
Katika kesi ya msingi, washtakiwa walikuwa ni
Zombe, ASP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, Konstebo Noel Leonard,
Konstebo Jane Andrew, Koplo Nyangerela Moris, Konstebo Emmanuel Mabula
na Koplo Felix Sedrick,
Wengine walikuwa ni Konstebo Michael Shonza,
Koplo Abeneth Saro, Koplo Rashid Lema (aliyefariki kabla ya kujitetea),
Koplo Rajabu Bakari na Koplo Festus Gwabisabi.
Washtakiwa hao walikuwa wakidaiwa kuwa Januari
14, 2006, katika Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam,
waliwaua kwa makusudi wafanyabiashara watatu wa madini, waliokwenda
kuuza madini yao Dar es Salaam na dereva teksi aliyekuwa akiwaendesha.
Wafanyabiashara hao ni Sabinus Chigumbi,
‘Jongo’ na ndugu yake Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe pamoja na Juma
Ndugu, ambaye alikuwa dereva teksi.
Awali, washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa
13, lakini hadi ilipotolewa hukumu, walikuwa wamebakia tisa tu, baada ya
wengine watatu kuachiwa huru katika hatua ya awali na mmoja kufariki
dunia.
Washtakiwa walioachiwa huru ni Konstebo
Leonard, Koplo Moris na Koplo Sedrick walioachiwa huru kabla ya hatua ya
kujitetea baada ya kuonekana kuwa hawana kesi ya kujibu.
Pia Koplo Lema, licha ya kuwa miongoni mwa
washtakiwa waliopatikana na kesi ya kujibu, alifariki dunia, wakati
wenzake wakiwa wameshaanza kujitetea.
Hata hivyo, Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam, iliwaachia huru washtakiwa wote ikisema kuwa
baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote,
imeridhika kuwa washtakiwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa
yakiwakabili.
Hata hivyo, siku chache baada ya kuachiwa
huru, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), alikata rufaa Mahakama ya Rufani,
akipinga hukumu ya Mahakama Kuu. Katika rufani hiyo DPP alidai kuwa Jaji
Salum Massati aliyetoa hukumu hiyo, alikosea kuwaachia huru washtakiwa
hao kwani kulikuwa na ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani.
Katika hukumu hiyo, Jaji Massati aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo
alisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi
ya washtakiwa hao bila kuacha shaka.
Pia Jaji Massati alisema kuwa amebaini kuwa
wauaji halisi hawajafikishwa mahakamani na kwamba kutokana na kutokuwapo
kwao mahakamani, mashtaka dhidi ya washtakwa waliokuwapo mahakamani
hayawezi kutengenezeka, hivyo akaiagiza Jamhuri kuwasaka na kuwafikisha
mahakamani wauaji halisi.
DPP katika rufaa hiyo namba 254/2009,
iliyofunguliwa Oktoba 6, 2009, amebainisha sababu kumi na moja ambazo
zimemfanya apinge hukumu hiyo yote, akidai kwamba kwa mujibu wa ushahidi
uliotolewa mahakamani, washtakiwa wote walikuwa na hatia.
Katika hoja hizo za rufaa, DPP amedokeza kile alichokiita upungufu katika hukumu hiyo, kwa kila mshtakiwa.
Katika rufaa hiyo, DPP katika hoja zake anadai
kuwa jaji alipotoka, alishindwa kutafsiri sheria na kanuni mbalimbali
zinazohusu mashtaka ya jinai na kwamba alijichanganya katika hukumu
hiyo.
CHANZO: MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment