Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

TBL YASHINDA TUZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI SEKTA YA VIWANDA

Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka (kushoto), akimkabidhi tuzo Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, baada ya kampuni hiyo kushinda masuala ya usalama mahali pa kazi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama kazini duniani, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Makongoro Mahanga.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akimpongeza , Renatus Nyanda kwa niaba ya TBL.
Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kabaka pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo hizo.

HALMASHAURI YA WILAYA YA ILALA YAPITISHA BAJETI YA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 90.


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, wakati akisoma bajeti ya zaidi ya sh.bilioni 93.5 iliyopitishwa na Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2012-2013. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Kijamii Angelina Malembeka na Naibu Meya Kheri Kessy. (Na Mpiga Picha Wetu).

TBL YASHINDA TUZO YA USALAMA MAHALA PA KAZI SEKTA YA VIWANDAWaziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudentia Kabaka (kushoto), akimkabidhi tuzo Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda, baada ya kampuni hiyo kushinda masuala ya usalama mahali pa kazi, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Afya na Usalama kazini duniani, Dar es Salaam juzi. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Makongoro Mahanga.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) akimpongeza , Renatus Nyanda kwa niaba ya TBL.
Meneja Usalama Mahala pa Kazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Renatus Nyanda (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Kabaka pamoja na baadhi ya washindi wa tuzo hizo.

SIMU AINA YA NOKIA ASHA YAZINDULIWA JIJINI DAR KWA KISHINDO


Meneja wa
Nokia Nchini Tanzania, Samson Majwala (kushoto) akitoa zawadi ya Simu ya Nokia “Asha”
kwa Dj Fetty wa Radio Cloudz wakati wa uzinduzi  wa simu ya Nokia ”Asha” 200,302,303,
uliofanyika kwenye Klabu ya Billicanas Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
 

Wasanii
wa kundi la Tanzania House of Talent (THT) wakicheza wakati wa uzinduzi wa simu
ya Nokia ”Asha” 200,302,303, uliofanyika kwenye Klabu ya Billicanas Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki
 
Balozi
wa Nokia “Asha”, Rachel Samweli (katikati) akiwaelekeza wateja ubora wa simu
hiyo wakati wa uzinduzi wa simu ya Nokia ”Asha” 200,302,303, uliofanyika kwenye
Klabu ya Billicanas Dar es Salaam


THT wakicheza


Balozi
wa Nokia “Asha”, Rachel Samweli (katikati) akiwaelekeza wateja ubora wa simu
hiyo wakati wa uzinduzi wa simu ya Nokia ”Asha” 200,302,303, uliofanyika kwenye
Klabu ya Billicanas Dar es SalaamBalozi
wa Nokia “Asha”, Abdalah Ngoma (wa pili kulia) akiwaelekeza wateja ubora wa
simu hiyo wakati wa uzinduzi wa simu ya Nokia ”Asha” 200,302,303, uliofanyika
kwenye Klabu ya Billicanas Dar es Salaam


Mtangazaji na Dj
wa Radio ya Cloudz fm, Fatuma Hassan(Fetty), (kulia) akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa simu ya Nokia ”Asha” 200,302,303,
uliofanyika kwenye Klabu ya Billicanas Dar es Salaam .Kushoto ni
Mtangazaji wa Radio ya East Afrika,Anna Peter,na mtangazaji wa Radio
Cloudz, Hamis Mandi(B12 


 Meneja wa
Nokia Nchini Tanzania, Samson Majwala (kushoto) akitoa zawadi ya Simu ya Nokia “Asha”kwa
Mtangazaji wa Radio ya East Afrika,Anna Peter
.
 Wakiwa na furaha mara baada ya kupata zawadi ya simu


 Sasa muziki kwenda mbeleWadau wakisakata rumba kwa kwenda mbele.

Picha Na Michael Machellah

Miss Ukonga na Miss Tabata wafanya mazoezi ya pamoja Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa
katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati
walipofanya mazoezi ya pamoja jana. 
  
WAREMBO
wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja
katika kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani
ya urembo.
Warembo
wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo
Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.

Vitongoji
vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika
Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss
Tanzania 2012.

Wakizungumza
jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa
Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho
wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa
kati wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.

“Tunawashukuiru
sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali
ambao ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao
tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.

Nae
Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya
kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na
kufnya nao mazoezi ya pamoja.

Mapema
Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao
kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.

Shindano
la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata
linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.


Washindi wa shindano la mwanamke mjasiliamali wakabidhiwa hundi zao jijini dar

Wanachama wa UWF wakiwa na baadhi ya washindi wa waliong'ara vizuri kwenye shindano la kumsaka Mwanamke Mjasiliamali,kupitia tuzo ya Mwanamakuka (lililofanyika March 8),na hatimaye kuwapata washindi watano wa tuzo hiyo.
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akimkabidhi Bi Nassra Mussa  hundi ya shilingi laki tano kwa kuibuka mshindi wa tano wa tuzo ya Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka.Pichani kulia ni  Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda.Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar
Muwakilishi wa Clouds FM,Abdull Mohamed akimkabidhi Bi.Joyce Mabula hundi ya shilindi laki saba unusu kwa kuibuka mshindi wa nne wa tuzo ya Mwanamke Mjasiliamali (tuzo ya Mwanamakuka). 
Baadhi ya Washindi wa shindano la Mwanamke Mjasiliamali kupitia tuzo ya Mwanamakuka wakifuatilia jambo
Meneja Miradi wa UWF,Bi.Mariam Shamo akizungumza machache mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo,iliyofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za UWF zilizopo Mikocheni, jijini Dar.
Mwenyekiti wa UWF,Bi Mwate Madinda akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo sambamba na wanachama wenyewe wa UWF.
Picha kwa Hisani ya Jiachie Blog

NHIF YAANZISHA KLABU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WAKE KILA J'MOSI KWENYE VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI OYSTERBAY


Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya wajiandaa na uzinduzi wa klabu ya michezo kwa watumishi wake ili kuwapa fursa ya kulinda afya zao na magonjwa mabalimbali yanayotokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha ya kila siku kama vile kisukari, shinikizo la damu na mengineyo mengi ambayo kwa kwa sasa yamekuwa tishio kwa maisha ya binadamu wa leo.

Akizungumza wakati wa mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Oyesterbay Meneja wa timu ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha rasilimali watu na utawala bi Jane nchimbi alisema 'Tumekuwa na utaratibu huu tangu mwanzoni mwa mwaka jana lakini kidogo tulikuwa tumebanwa na majukumu ,lakini kwa sasa tumeamua kwa pamoja kuufanya utaratibu huu kuwa endelevu kwani utasaidia kujenga afya hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wengi wa umma  tunatumia muda mwingi kwenye ofisini tukihudumia wateja hivyo kuwa na nafasi finyu kushiriki mazoezi kama ambavyo NHIF tumethubutu...

Mpango huu unawajumuhisha pia wale watumishi wa Mfuko kwenye ofisi  za Mkoani, mpango wa baadaye ni kuwa na eneo maalum la kufanyia mazoezi (gym) ili huduma zote za msingi ziweze kupatikana.alisema Bi Jane kijazi

Naye nahodha wa timu ya mpira wa pete  ya NHIF bi Sabina Komba  ……aliwataka wafanyakazi wanaoshiriki mazoezi kwenye klabu hiyo kutambua kuwa wao ni mabalozi katika kuhamasisha wananchi na wananchama wa mfuko huo kupenda na kuthamini michezo kwani mfumo wa maisha ya kisasa umegubikwa na maradhi mengi na  makubwa ambayo yanaathiri afya zetu na walio wengi

VIJANA WA ELIMU YA JUU WATINGA CCM KUFIKISHA UJUMBE WAO DHIDI YA MAFISADI

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza na vijana wa Shirikisho la CCM la vijana wa CCM wlioko vyuo vya Elimu ya Juu, walipofika leo kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Dar es Salaam, kumfikishia ujumbe wao kuhusu mawaziri na watumishi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na upotefu wa fedha za umma.
Nape akisoma ujumbe uliloonyesha kumvutia zaidi kwenye moja ya mabango ya wanavyuo hao.
Vijana hao wakionyesha bango lenye ujumbe mahsusi kuhusu maana ya Mapinduzi.
Vijana wakionyesha bango la kuwataka 'magamba' waendelee kujitoa CCM.
Nape akisoma ujumbe kwenye moja ya mabango waliyofika nayo wanafuvyo hao.
Wanavyuo wakionyesha bango la kuwataka wasaidizi wa Rais kuwajibika inapobidi.
Picha kwa Hisani ya Michuzi Blog

TGNP yatoa madai ya Jumla katika Katiba MpyaBaadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana katika Hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wahariri katika semina hiyo.
Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Nevilli Meena (kushoto) akijadiliana jambo na Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi. Kulia ni mmoja wa maofisa wa TGNP kutoka kitengo cha Habari.
Picha ya pamoja kati ya wahariri mbalimbali walioshiriki katika semina hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya (wa kwanza kulia aliyechuchumaa).

Na Joachim Mushi,Dar es Salaam

MTANDO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetoa maoni ya jumla ambayo wangependa yaingizwe kwenye mchakato wa uundwaji wa Katiba Mpya ya Tanzania. Maoni hayo yalitolewa na TGNP kwenye semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam katika semina hiyo, Mratibu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa TGNP, Bi. Lilian Liundi alisema madaraka katika muhimili wa utawala wa sasa ni makubwa hivyo kushauri yapunguzwe na kuwe na utengano kati ya mihimili mikuu mitatu ya nchi.

Bi. Liundi pia ametaka uwepo wa uwiano sawa wa kijinsia (50/50) huku akitaka mawaziri wasiwe wabunge na uwepo wa utaratibu wa viongozi (wabunge, madiwani) kuwajibishwa katikati ya mihula tofauti na ilivyo sasa.

Aidha mambo mengine ambayo Bi. Liundi ameyatoa kama changamoto na kushauri yaingizwe kwenye mchakato wa Katiba Mpya ni pamoja na kufutwa kwa adhabu, uwepo wa uhuru wa kupinga matokeo ya urais baada ya kutangazwa na ukomo wa uongozi wa wabunge, madiwani na serikali za mitaa.

Amesema siasa za uliberali mamboleo zilizoletwa na mataifa ya nje katika nchi za kiafrika zimesababisha mtafaruku mkubwa katika siasa za kiafrika, hali ambayo imezua migomo na mapambano dhidi ya uporaji wa rasilimali, ubinafsishaji wa huduma za afya na kuzifanya kama bidhaa na uporaji mkubwa wa ardhi na madini.

“Harakati hizi zimesababisha makundi ya kijamii, vyama vya siasa na wanaharakati kuanza kudai mabadiliko ya katiba katika nchi zao. Mfano mzuri ni nchini Kenya 2007,” alisema.

Pamoja na hayo alisema licha ya mchango mkubwa unaotolewa na wanawake nchini Tanzania bado hakuna fursa sawa kimgawanyo wa masuala mbalimbali.

Asilimia 80 ya nguvu kazi vijijini ni wanawake na asilimia 60 yao ni wazalishaji wa chakula. Wanawake ambao hawana ajira ni asilimia 40.3 (2006) ukilinganisha na wanaume ambao walikuwa asilimia 19.2 ( 2006), asilimia 66 ya wanawake wanafanya kazi zisizokuwa na kipato (kazi za huduma)... asilimia 39.5 ya wanawake hawajasoma ukilinganisha na asilimia 25.3 ya wanaume...,”

Awali akitoa mada katika semina hiyo ya wahariri, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Usu Mallya alisema licha ya uwepo wa maendeleo kwa kiasi fulani ukilinganisha na miaka ya nyuma, bado kuna mifumo kandamizi inayoikabili jamii ya kipato cha chini.

Alisema maendeleo ya huduma za jamii katika maeneo mbalimbali kwa kiasi kikubwa yanawanufaisha zaidi wenye nacho (matajiri) na si masikini. “Huduma za jamii zimeongezeka ndiyo lakini wanaonufaika zaidi na huduma hizo ni wachache...ukiangalia utaona Serikali inawajibika zaidi kwa wafadhili na si wananchi wake...,” alisema Bi. Mallya.

Alioneza kwa sasa hata tabaka la wasionacho na walionacho ni kubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma huku jukumu la kuihudumia jamii likirudi kwa familia zenyewe (majumbani) na si Serikali walioiweka madarakani kuwahudumia wananchi wake

Live !Kutoka uwanja wa Taifa mechi kati ya Simba vs Shandy

Shabiki akionesha mambo ni Tatu bila 
Picha zote na Gadner Dibibi 
Endelea kufuatilia

Siku Ya Usalama Wa Afya Duniani


Waziri wa Kazi na Ajia, Mh Gaundentia Kabaka, akimkabidhi ngao, Mkurugenzi Mtendaji wa Songas,baada ya kampuni ya Songas kuwa Mshindi wa kwanza katika sekta ya nishati na pia mshindi wa jumla wa mashindano maalumu yaliyoandaliwa na Wakala wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi (OSHA) ,wakati wa maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya duniani yaliyofanyika Kitaifa katika Ukumbi wa Mliman City Dar es salaam
wafanyakazi kutoka kampuni ya Geita Gold Mine wakifuatilia kwa umakini, baadhi ya maada ambazo zilikuwa zikijadiliwa na wataalamu wa usalama na afya sehemu za kazi, kutoka ILO,OSHA, na watalaamu toka chuo kikuu cha Dar es salaam,
mmoja wa washiriki wa maonesho ambayo yalikuwa yakieendelea sambamba na maadhimisho ya siku ya usalama na Afya duniani, akikabidhiwa cheti cha ushiriki wa maonesho toka kwa Waziri wa kazi na Ajira, Mh Gaundentia Kabaka
Waziri wa Kazi na Ajira katikati akiwa na washindi mbalimbali wa TUZO maalumu, iliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) wakati wa Maadhimisho ya Siku ya usalama na Afya duniani Kitaifa Mlimani City Dar es Salaam,wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa ILO hapa nchini ndugu Alex Musindo, wa pili kushoto mstari wa nyuma ni Dr Makongoro Mahanga na Katibu mkuu wa Wizara ya kazi na ajira ndugu Eric Shitindi, pamoja na wajumbe wa bdoi ya ushauri wa wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHAA) na Mtendaji mkuu wa OSHA Dr Akwilina Kayumba.

 duniani kote, wafanyakazi huadhimisha siku ya usalama na afya duniani, siku hii ni maalumu kwa ajili ya kuwakumbuka ndugu zetu waliopatwa na magonjwa ajali ama kupoteza maisha wakiwa makazini.OSHA ambayo wakala mwenye wajibu wa kusimamia sheria ya usalama na Afya mahali pa kazi iliandaa kongamano la wataaluma mbalimbali kuhusiana na siku hii maalumu
 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa