Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
Jeneza lenye mwili wa marehemu Sadick Juma Kilowoko a.k.a Sajuki ukiwasili kwenye makaburi ya Kisutu,Upanga jijini Dar kwa ajili ya mazishi.
Baadhi ya watu waliofika kwenye mazishi ya marehemu sajuki jioni ya leo Kisutu,jijini dar.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh Zitto Kabwe akifafanua jambo mbele ya baadhi ya Wanahabari kabla ya mazishi ya marehemu Sajuki,yaliyofanyika leo Kisutu jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na maelfi ya watu.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza jambo na Meya wa Wilaya ya Ilala,Mh Jerry Silaa ,shoto ni Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu nchini,Simon Mwakifwamba akisikiliza .
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki (pichani shoto) wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.Pichani kati Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu nchini,Simon Mwakifwamba na mwisho kabisa Meya ya Wilaya ya Ilala,Mh Jerry Silaa.
Mwandishi mkongwe wa kampuni ya Uhuru Publications akiitafusta taswira murua kabisa kwenye mazishi ya marehemu Sajuki,yaliyoongozwa na Rais Kikwete mapema leo jioni kwenye makaburi ya Kisutu,Upanga jijini Dar.
Baadhi ndugu jamaa na marafiki waliofika kwenye mazsishi ya marehemu Sajuki,wakisubiri mwili wake waupokee kwa ajili ya maziko.
PICHA NA IKULU
PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment