Home » » HATARI SANA : MAMLAKA YA MAJI SAFI NA TAKA (DAWASCO) JIJINI DAR ES SALAAM , MNAIONA HALI HII YA UCHAFU NA MIPASUKO HII? JIJI MPO? SHUHUDIA

HATARI SANA : MAMLAKA YA MAJI SAFI NA TAKA (DAWASCO) JIJINI DAR ES SALAAM , MNAIONA HALI HII YA UCHAFU NA MIPASUKO HII? JIJI MPO? SHUHUDIA

 HUU NI UCHAFU AMBAO UMEKITHIRI SANA KATIKA ENEO HILI AMBAPO  KILA MTU ANATUPA TAKA HAPO.
 HAPA KUNA MPASUKO WA BOMBA AU SIM TANK LA MAJI TAKA  AMBALO LINALETA MAJI MACHAFU NA KUELEKEA MTONI
 HUWEZI AMINI PEMBENI YA HUU UCHAFU MKUBWA KUNA WATU WANAISHI, NA ZAIDI WAPO HAWANA WASI WASI
 HAYA NI MAMIZIGO YA MAUCHAFU AMBAYO HUTUPIWA ENEO HILI HASA NYAKATI ZA USIKU,NA HAPA BOMBA HILI AU TANK LA MAJI  TAKA LIMEFUMUKA NA KUELEKEZA MAJI MTONI AMBAO NAO NI MCHAFU ZAIDI
 HUU NI MTO AMBAO NAO UMECHAFUKA MPAKA UMEBAKI KAMA MATOPE NA MAJI YAKE YANAELEKEZEWA HUKO BAHARI YA HINDI.
 HAYA NI MAJI AMBAYO YANATOKA KATIKA MOJA YA KIWANDA NA KUELEKEA KATIKA MTO HUO

 MFEREJI HUU NI MCHAFU SANA LAKINI CHA AJABU PEMBEZONI KUNA WATU WANAPIKA

 HIKI NI KIBANDA AMBACHO KWA UKWELI KIPO JIRANI KABISA NA MAJI TAKA , LAKINI WANACHI WANAPIKIWA CHAKULA HAPO NA KULA BILA KUHOFIA MAGONJWA YA MRIPUKO
HILI ENEO LIPO JIRANI KABISA NA BOMBA/TANK YA MAJI CHAFU PIA KUNA DAMPO LA MATAKA TAKA HATARISHI NA MTO MCHAFU SANA LAKINI WAKAZI WA ENEO HILO WAMEJENGA NA WANAISHI HAPO , KAMA NGUO ZINAVYO ONEKANA.


**************************************

KAMERA YA BLOGS ZA MIKOA LEO KATIKA PITA PITA ZAKE MAENEO YA JIJI LA DAR ES SALAAM , ILIBAINI KWAMBA KUNA ENEO  MOJA AMBALO WANANCHI WAMELIPIGIA KELELE MPAKA WAMECHOKA, ENEO HILO AMBALO LIMEKITHIRI KWA UCHAFU NA KUONESHA KUWA HAKUNA JITIHADA ZA WAHUSIKA WA AFYA KULIFANYIA KAZI HATA KUWEKA MKONO WAO WA KUSAFISHA, LIMEENDELEA KUWA CHAFU NA KUSABABISHA KERO KUBWA SANA HASA KWA WATU WANAO ISHI HAPO

WAKIZUNGUMZA NA BAADHI YA WAKAZI NA WAFANYAKAZI WA ENEO HILO, WAMEIAMBIA BLOGS ZA MIKOA KWAMBA WAMESHA LALAMIKA SANA NA KULAUMU LAKINI HAKUNA JITIHADA ZOZOTE ZIMEFANYIKA ILI KUNUSURU ENEO HILO NA KULISAFISHA.

MKAZI MMOJA WA ENEO HILO AMBAYE HAKUTAKA KUTAJWA JINA LAKE ALISEMA KWAMBA " ENEO HILI LIMESHA PIGIWA SANA KELELE, HASA MIMI KUANZIA NIFIKE HAPA NIMELIONA HILO BOMBA SIJUI SIMTANK AU BOMBA LIMEPASUKA NA HAKUNA JITIHADA ZOZOTE ZINAZO FANYIKA KUBOMOA NA KUDHIBITI HAPA"

MKAZI MWENGINE ANAYE ISHI KATIKA ENEO HILO ALISEMA "NAWASHANGAA SANA HATA HAWA WALIOJENGA NA KUUZA CHAKULA ENEO HILI BILAKIJALI AFYA ZA WANAO WAUZIA"

JUHUDI ZA KUWATAFUTA WAHUSIKA ZINAFANYIKA 

SWALI NI JE UCHAFU HUU ULIOPILIZA KIASI  JIJI HAWAUONI? NA JE KUPASUKA KWA BOMBA HILI WAHUSIKA WA MAJI TAKA NA SAFI HAWAONI? NA JE WATU WA AFYA KUNA MAENEO HAWATEMBELEI KUTAZAMA HALI IKOJE?

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa