Home » » MISS UTALII TANZANIA VIPAJI 2012/13 KUPATIKANA KESHO DAR LIVE

MISS UTALII TANZANIA VIPAJI 2012/13 KUPATIKANA KESHO DAR LIVE



Shindano
la Taifa la Miss Utalii Vipaji 2012/13
linafanyika kesho katika ukumbi wa Dar Live Mbagala, ambapo Warembo  40 kutoka Tanzania Bara, Zanzibar na Kanda
Maalum vyuo Vikuu Tanzania , watapanda stejini kushindana kucheza Ngoma za
asili  kutoka Mikoa ambayo wanawakirisha,watapita
na mavazi mbalimbali.
Katika
shindano hilo mbali na Burudani kutoka kwa Warembo wa Miss Utalii Tanzania
2012/13  kutakuwa na Burudani zaidi za
Ngoma za Asili, Muziki wa kizazi Kipya pamoja na Burudani kutoka kwa Mwanamuziki
wa Kimataifa Che Mundugwao, Atakuwepo pia mwanamuziki chipukizi wa Bongo Flava
Dogo Genius ambeye ametokea kuwa mpinzani mkubwa wa Dogo Janja na Asley.

Shindano
hili ni la awali ambalo litapata Mshindi wa Vipaji kabla ya kufanyika fainali
kuu ambalo litampata Miss Utalii Tanzania litakalo Fanyika Tarehe 17.03.2013
katika ukumbi wa Dar Live. Mshindi wa Tuzo hilo la Vipaji atajipatia zawadi ya
Kusomeshwa Bure katika ngazi ya Cheti au Diploma kulingana na Sifa zake.
Mshindi wa Mwaka jana na ambaye anashikiria taji Hilo kwa sasa ni Daisy
Msumbusi Miss Utalii Kutoka Mkoa wa Kagera.

Katika
Shindano hilo , ulinzi utakuwa umeimarishwa ambapo kutakuwa na Polisi na Ninja,
usalama wa Magari pamoja na vitu vyote
utakuwa ni wakutosha, kutakuwa na eneo la kutosha la kuegesha Magari na
walinzi muda wote watakuwepo katika eneo hilo.
Viingilio
katika Shindano hilo itakuwa kama ifuatavyo, Viti vya kawaida Tsh 5,000 na Viti
Maalum 10,000

Fainali
za Taifa za Miss Utalii Tanzania mwaka huu Zimedhamiwa na: Mtwana Catering
Services, Ikondolelo Lodge, Zizou Fashion, Coca Cola Kwanza, VAM General
Suppries Limited,Michuzi Media Group,Global Publishers, TANAPA, Ngorongoro
Crater, Lakeland Africa, Clouds Media Group, Star Tv, Vailey Spring,Dotinata
Decoration,Tone Multimedia Group, Baraza la sanaa la Taifa (BASATA )
www.misstourismorganisation.blogspot.com


0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa