Baadhi ya majengo ya ghorofa yaliyopo jijini Dar es Salaam
Dar es Salaam. Imebainika kuwa nyumba nyingi zilizopo jijini Dar
es Salaam na maeneo mengine ya nchi, zipo hatarini kubomoka kutokana na
kujengwa kwa matofali yasiyokuwa na ubora.
Pia, hatua hiyo inatokana na kutokuwapo kwa
ukaguzi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi yakiwamo matofali ya saruji
yanayotumika katika ujenzi wa nyumba hizo.
Uchunguzi uliyofanywa na Mwananchi hivi karibuni
jijini Dar es Salaam na baadhi ya maeneo nchini, umebaini kuwepo kwa
ongezeko kubwa la biashara holela ya matofali yanayotengezwa kwa ubora
hafifu.
Uchunguzi pia unaonyesha kutokuwapo kwa usimamizi
wa kutosha katika sekta ya ujenzi nchini ni moja ya vyanzo vya watu
kufanya biashara ya vifaa vya ujenzi kiholela.
Biashara hizo ni pamoja na uuzaji wa matofali yasiyokuwa na viwango kutokana na kukosa udhibiti maalumu.
Biashara hizo ni pamoja na uuzaji wa matofali yasiyokuwa na viwango kutokana na kukosa udhibiti maalumu.
Moja ya mambo yanayosababisha matofali
yanayotumika katika ujenzi jijini Dar es Salaam kuonekana kuwa hayana
ubora ni utengenezaji wa matofali hayo.
Imegundulika kuwa saruji inayotumika katika
utengenezaji huo ni ndogo na mchanga unakuwa mwingi kwa lengo la
kutengeneza matofali mengi ili kupata faida.
Wakati uchunguzi huo ukionyesha hivyo Mwananchi,
ilimtafuta Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Mhandisi
Boniface Muhegi, ambaye alishauri kufanyika kwa uchunguzi wa bidhaa
zinazotumika katika ujenzi.
Muhegi anasema “Ili kuepusha madhara hasa kuanguka
kwa majengo ni vyema Shirika la Viwango Tanzania (TBS), likachukua
hatua ya kufanya ukaguzi wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi ili
kuongeza usalama katika masuala ya ujenzi.|
Anasema ili kuhakikisha kuwa majengo yanakuwa
salama, ni vyema watu wakatumia wakandarasi waliosajiliwa ili kuwabana
wakati kunapotokea madhara.
“Sisi tunashauri kwamba kama mtu anataka kujenga
nyumba amayo ni salama, ni vyema akatumia wakandarasi waliosajiliwa ili
iwe rahisi kuwabana wakati tatizo lolote linapojitokeza,”anasema.
Mhandisi Muhegi anasema “Ni vyema wananchi nao
wakatambua kwamba matumizi ya vifaa visivyokuwa na viwango sio salama
kwa maisha yao”.
Anasema kila mmoja aone haja ya kutumia vifaa
vyenye ubora ili kujihakikishia usalama wa makazi yake na kuepusha
kutokea kwa majanga mbalimbali.
SOMA ZAIDI HAPA MWANANCHI GAZETI
SOMA ZAIDI HAPA MWANANCHI GAZETI
0 comments:
Post a Comment