Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani nchini Dk. Emmanuel Nchimbi,
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw.
Richard Ragan na Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) wakitoa heshima kwa wimbo wa mataifa kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani
Dk. Emmanuel Nchimbi akiwasili kwenye Mnara wa Mashujaa viwanja vya
Mnazi Mmoja katika maadhimisho ya kumbukumbu ya Askari wa Kulinda amani
wa Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali pamoja viongozi wa dini.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula
Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiwasili kwenye viwanja
hivyo jijini Dar es Salaam kushiriki kwenye maadhimisho ya kumbukumbu
ya Askari wa Kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Mgeni rasmi Waziri Mambo ya Ndani
nchini Dk. Emmanuel Nchimbi akielekea kuweka shada la maua kwenye Mnara
wa Mashujaa ikiwa ni ishara ya kuwakumbuka askari wa kulinda Amani wa
Umoja wa Mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akiweka
shada la maua kwenye Mnara wa kumbukumbu ya Mashujaa uliopo katika
viwanja vya Mnazi Mmoja wakati wa maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa
Kulinda Amani wa Umoja wa mataifa walipoteza maisha wakiwa kazini.
Mgeni rasmi Mh. Dk. Emmanuel Nchimbi akitoa heshima mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara huo.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula
Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akielekea kuweka shada
la maua kwenye maadhimisho ya kuwakumbuka Askari wa Kulinda Amani wa
Umoja wa Mataifa yaliyofanyika leo kwenye mnara wa kumbukumbu ya
Mashujaa uliopo viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akiweka shada la maua kwenye mnara huo.
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) akiweka shada la maua kwenye mnara wa
kumbukumbu ya Mashujaa kwa niaba ya Meja Jenerali Salum Mustafa Kijuu
wakati wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka Askari wa kulinda Amani wa
Umoja wa mataifa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja leo.
Kanali Dominic Mrope wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) akitoa heshima zake mara baada ya kuweka shada la maua.
Mmoja wa askari wa JWTZ akipendisha
bendera ya Umoja wa Mataifa kama ishara ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja
huo wanaolinda Amani katika nchi mbalimbali za Afrika.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani
Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wageni waalikwa wakati wa
maadhimisho ya kuwakumba Askari wa Umoja wa mataifa wa Kulinda Amani
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Shirika la Chakula
Duniani nchini Tanzania (WFP) Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya
Mratibu Kazi wa Umoja wa Mataifa hapa nchini Dk. Alberic Kacou kwenye
maadhimisho ya Siku ya kumbukumbu ya Askari wa Umoja wa Mataifa wa
kulinda Amani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Na Mwandishi wetu.
Tanzania imesema shughuli ya
operesheni za kulinda amani katika mataifa yenye mvutano wa kivita
barani Afrika zinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upelekwaji
wa wanajeshi na udhibiti wa rasilimali na utoaji wa maamuzi.
Akizungumza katika maadhimisho ya
Siku ya Kimataifa ya Kuwakumbuka Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa
yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar e s Salaam,
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Emmanuel Nchimbi amesema
tunapoadhimisha siku hii pia tunawakumbuka raia, askari na wapiganaji
zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha tangu mwaka 1948 wakiwa katika zoezi
la kulinda amani.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Chakula
Duniani nchini Tanzania Bw. Richard Ragan akizungumza kwa niaba ya
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alberic Kacou amepongeza vikosi
vya Jeshi la wananchi wa Tanzania na Polisi wa Usalama wa Raia kwa
kuandaa tukio hilo la kumbukumbu ya walinda amani wa Umoja wa mataifa
wake kwa waume waliopoteza maisha yao.
Amesema katika siku hii ya kimataifa,
tuitumie kuwakumbuka walinda amani zaidi ya 3,100 waliopoteza maisha na
kuwaunga mkono askari zaidi ya 111,000 waliopo na wanaoendelea kulinda
amani katika nchi mbalimbali zilizo na migogoro.
Kwa hisani ya Father Kidevu Blog
0 comments:
Post a Comment